Benki ya NMB tawi la Nyasa hivi karibuni limetoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya tsh milioni tano katika Shule ya msingi Kilosa iliyopo kata ya kilosa na Sekondari ya Monika Mbega katika kata ya Mbaha Wilayani hapa ili kuboresha miundombinu ya shule hizo na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi msaada huo katika shule hizo kwa mkuu wa wilaya ya Nyasa mh.Isabela chilumba meneja wa Benki ya NMB Tawi la Nyasa kennedy Chinguile amesema Benki ya Nmb kwa kuona umuhimu wa sekta ya elimu na kuunga juhudi za Serikali za kuboresha elimu imeamua kutenga aslilimia moja ya faida wanayopata ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii inayowazunguka.
Chinguile aliitaja msaada waliotoa kwa shule ya msingi Kilosa kuwa ni Bati mia moja nondo 30 ml 12 simenti mifuko hamsini(50) misumari ya bati kilo 50 chokaa mifuko kumi rangi ya maji lita 20 ndoo 4,nondo ndogo ml 6 wirenesh 11 vifaa vyote vikiwa na thamani ya tsh milioni tano,na shule ya Sekondari ya Monika Mbega ni bati 162 misumari kilo themanini(80),misumari ya inchi tatu kilo 25 vifaa vyenye thamani ya tsh milioni tano na kufanya jumla ya msaada waliotoa ni tsh milioni kumi.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Dkt Oscar Mbyuzi wakati akimkaribisaha mgeni rasmi aliwashukuru sana Nmb kwa kutatua changamoto zilizowakabili kwa muda mrefu za kukabiliana na ujenzi wa miundombinu katika shule mbalimbali za Wilaya ya Nyasa na kuhakikisha kuwa halmashauri inakuwa na majengo mazuri yanayomvutia mwanafunzi kujifunza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba ameipongeza benki ya Nmb Tawi la Nyasa kwa kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu hivyo itasaidia hususani katika shule ambazo Nmb wamezipa msaada huo wa vifaa vya ujenzi ambavyo kweli ilikuwa nia changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili na kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa anatoa shukrani za dhati kwa meneja wa Nmb tawi la Nyasa na akatoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuiga mfano wa Nmb Tawi la Nyasa kwa kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha elimu inastawi katika maeneo yetu.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa