Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amepokea vifaa vyenye thamani ya Mil. 100.9 kutoka kwa wadau wa Benki ya NMB vifaa ambavyo vitasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati kwenye shule za Msingi, na afya Mkoani Ruvuma.
Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambalpo limefanyika tarehe 22 januari 2024 katika uwanja vya shule ya Msingi Kibulang’oma ambapo walihuhudhuria wakuu wa Wilaya wote, Wakurugenzi pamoja na Wadau wa Nmb kwa lengo la kukabidhi madawati hayo.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye tukio hio ambapo amewataka walimu kuhakikisha wanasimamia na kulinda vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu.
Akizungumza Meneja wa Benki NMB Kanda Bi Faraja Ng’ingo alisema NMB kwa kutambua umuhimu wa wateja wao wameweka utaratibu wa kurudisha asilimia za faida kwa wateja wao ambapo kila mwaka hununua madawati kwa shule za Msingi na Sekondari, Afya na huduma nyinginezo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa