Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa inatarajia kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambayo inatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni moja na nusu (1,500,000,000) itakayojengwa katika kitongoji cha Mtambo wa Lami kijiji cha Nangombo Kata ya Kilosa wilayani hapa ili kuwasogezea karibu huduma ya matibabu wananchi wa Wilaya ya Nyasa.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Dkt Oscar Mbyuzi wakati akiongea na wananchi wa Kitongoji cha Mtambo wa Lami, kijiji cha Nangombo Kata ya Kilosa, wakati akiwapa taarifa ya kukamilika kwa Taratibu kwa kuanza ujenzi wa majengo saba ya Hospitali ya Wilaya ya Wilaya ya Nyasa.
Dkt Mbyuzi alifafanua kuwa Wilaya ya Nyasa inakusudia kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya itakayojengwa katika kitongoji cha Mtambo wa lami katika kijiji cha Nangombo Kata ya kilosa ujenzi ambao unatarajia kuanza kesho kwa kusogeza miundombinu ya maji na kuanza ujenzi huo mara moja kwa kuwa tayari serikali imeshaleta fedha kiasi cha tsh (1,500,000,0000/=) bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujezi wa hospitali hiyo.
Aliyataja majengo yanayaoanza kujenga kuwa ni Jengo la utawala,Jengo la wagonjwa wan je(OPD),Jengo la stoo ya Dawa,Jengo la Maabara,jengo la vipimo vya mionzi(x-ray)Jengo la kufulia nguo(Laundry) na jengo la wazazi.
Aliongeza kuwa Taratibu zote za kuanza ujenzi zimekamilika ikiwa ni pamoja na kutangaza matangazo ya kutafuta fundi wa kujenga majengo ya hospitali hiyo na kuwashirikisha wananchi wa wilaya hii ili washiriki kikamilifu katika zoezi hili la ujenzi wa hospitali kwa kuwa kuna mafundi kujenga na wafanyakazi mbalimbali watahitajika na kipaumbele kitatolewa kwa wakazi wa wilaya ya Nyasa ili waweze kufanya kazi na kuongeza kipato kupitia kazi mbalimbali watakazokuwa wanazifanya katika eneo hilo la ujenzi.
Hapo awali Wilaya ya Nyasa ilikuwa haina Hospitali ya Wilaya hivyo ilikuwa inawalazimu wananchi kutembea umbali wa kilometa 66 kwenda Hospitali ya Wilaya ya Mbinga kupata huduma za afya kwa kuwa hapa Nyasa kulikuwa na kituo cha afya cha Mbamba-bay ambacho kilikuwa hakiwezi kutoa huduma za afya zinazopatikana katika Hospitali za Wilaya.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia na Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwa amewajali sana wananchi wa Nyasa na hivyo kuwaondolea kero ya kupata matibabu mbali na nyasa hivyo aliahidi kusimamia vizuri ujenzi huu na kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuwaondolea kero wananchi wanaotembea umbali wa kilometa 66 kufuata huduma hizo kati hospitali ya wilaya ya Mbinga na kuongeza msongamano wa hali ya juu katika Hospitali hiyo.
“Namshukuru sana mheshimiwa Rais kwa kunipa fedha za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nyasa ambayo itawasaidia wananchi wangu kwa kuwa walikuwa wakiteseka wakisafiri takribani kilometa 66 kufuata matibabu katika wilaya ya mbinga kama unavojua mtu akiumwa atalazimika kutafuta nauli na kutembea umbali mrefu kufuata matibabu katika hospitali ya Wilaya hasa akina mama wajawazito ambao mara baada ya kukamilika hospitali ya Wilaya ya Nyasa itawaondolea usumbufu huo”.
Mhandisi Manyanya bado aliomwomba Rais kuona uwezekano wa kumwongezea fedha za ujenzi wa kituo kimoja cha afya katika kata ya Kingerikiti tarafa ya Mpepo ambapo kuna ongezeko kubwa la watu na wanauhitaji mkubwa wa kituo hicho cha afya. wakati akiwa katika ziara ya siku kumi katika Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa hivi karibuni wananchi wa kata ya Kingerikiti kupitia kwa Diwani wao wa kata ya kingerikiti mh. Alto Komba walimwomba Mbunge Manyanya kuwajengea kituo cha afya kwa kuwa nao wanapata mbali huduma za afya.
IMETOLEWA NA
NETHO C.SICHALI
AFISA HABARI
WILAYA YA NYASA
0743615706
TAREHE 24/01/2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa