MKOA wa Ruvuma umebarikiwa kuwa na vivutio adimu vya utalii wa okolojia na kiutamaduni ambao haufahamiki na wengi.Katika eneo la Masonya lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma lina utajiri wa utalii wa malikale na utambulisho wa Taifa kwa sababu katika eneo hili kuna nyumba yenye namba A 10 ambayo walikuwa wanafikia na kuishi Marais Hayati Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Samaro Machel wa Msumbiji kuanzia 1966 wakati wa harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Bartazar Nyamusya anasem viongozi hao pia walitumia kibanda unachokiona kama chumba cha mawasiliano na nchi zilizokuwa katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.Hata hivyo toka nyumba ya viongozi hadi kibanda hicho cha mawasiliano limejengwa handaki la chini kwa chini.Eneo la Masonya lipo kilometa 12 kaskazini mwa mji wa Tunduru.Eneo hili lenye ekari 100 linatakiwa kuendelezwa kwa sababu linaweza kutoa mchango mkubwa katika nyanja za utalii,uchumi,elimu na utafiti.Hata hivyo serikali katika eneo hili imejenga sekondari ya Masonya.
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo
Mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa