OFISI YA KATA MJIMWEMA YAGHARIMU milioni 25.5
MRADI wa ujenzi wa ofisi ya Kata Mjimwema iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umegharimu sh.milioni 25.56.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Stan Kibiki amesema kati ya fedha hizo nguvu ya wananchi ni shilingi 556,000 na gharama za serikali ni sh.milioni 25.
Amesema mradi wa ujenzi ya ofisi hiyo ulianza tangu mwaka wa fedha wa 2012/2013 ambapo amezitaja shughuli ambazo zilifanyika katika kipindi hicho kuwa ni kusafisha eneo la mradi,kujenga msingi na kunyanyua boma.
Kibiki amezitaja kazi ambazo zimefanyika katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kuwa ni kuweka ringbeam,kujenga sehemu zilizosalia na kuezeka.
Hata hivyo amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ametoa sh.milioni kumi kwa ajili ya ukamilishaji wa fedha katika hatua za utekelezaji ambapo anatoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kusaidia ili kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Kata ya Mjimwema yenye mitaa mitano ina jumla ya wakazi 12,469 kati yao wanaume ni 5603 na wanawake ni 6866.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa