Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali itakayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 22/09/2019 katika Manispaa ya Songea.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma Mkonge Ally akizungumza katika eneo la miradi hiyo ambayo ni; mradi wa Maji uliopo Luhila Kati, mradi wa ujenzi wa barabara ya Haf London Stand, mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya Matarawe, mradi wa kitalu nyumba uliopo Shule ya Sekondari Chandarua pamoja na mradi wa kituo cha afya kilichopo Bombambili, amewataka viongozi kuwa makini sana katika kufanya maandalizi ili waweze kufanikisha kupokea mwenge wa uhuru bila tatizo lolote.
Ally amewaomba kufanya marekebisho kwenyemiradi iliyo na mapungufumapema kabla ya tukio pia ametoa wito kwa viongozi kushirikiana katika kufanya maandalizi kwa kuwa mwenge wa uhuru una umuhimu zaidi kwa kuwa unajenga umoja na mshikamano kwa wananchi.
Viongozi wenzangu mwenge ni alama ya umoja.’’Amesema Mbeya.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mwenge wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Abraham Mwakalegule ameahidi kutekeleza na kuyafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru ili kufanikisha sauala hilo.
Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo amewashukuru kwa mchango wa mawazo ambayo yatasaidia kuzaa matokeo chanya katika maandalizi ya kupokea mwenge wa uhuru na amewaahidi kuwa wategemee mabadiliko mazuri katika sehemu zote zenye mapungufu.
“Hatutawaangusha tutakeleza kwa pamoja.” Amesema Sekambo
Mwenge wa uhuru ni alama ya umoja hivyo unapaswa kuwa wa taifa moja kama bendera na wimbo wa taifa.
Imeandaliwa na
Bacilius Kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Septemba 7, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa