Katibu Mkuu wa umoja wa wanunuzi mazao vijijini Mkoani Ruvuma Thadey Mwakaguo akizungumza katika mahojiano ofisini kwake mjini Songea,amesema bei ya Mahindi kwa mwaka huu inaridhisha ukilinganisha na msimu uliopita.
Bei ya mahindi katika msimu wa mwaka 2018/2019 imepanda kutoka shilingi 400 kwa kilo hadi kufikia shilingi 600 hali ambayo imeleta neema kwa wananchi wa wilayani Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujmla.
Kwa mujibu wa Mwakaguo,zao la mahindi kwa mwaka 2019 limeuzwa kwa asilimia 50 mwanzoni mwa msimu ukilinganisha na mwaka jana 2018 mauzo yalikuwa asilimia 50 kwa msimu mzima.
Mwakaguo amezitaja changamoto wanazopata katika soko lao kuwa ni kukosekana kwa maghala ya kuhifadhia mazao yao,wakulima kutozingatia ubora na viwango vya mazao wanayozalisha na kusababisha kushuka kwa soko hilo hali inayosababisha mazao kununuliwa kwa bei ya chini.
“Kutokana na kushuka kwa bei ya mahindi mwaka jana kulisababisha baadhi ya wakulima kususia na kukata tamaa kuzalisha zao hilo kwa wingi.”Amesema Mwakaguo
Hata Hivyo,Mjasiliamali Joseph Komba amesema kuwa suala la bei ya mazao kuwa nzuri lina manufaa kwa upande wao na kuomba Serikali kupunguza ushuru na kuwapa mikopo itakayowasaidia kuboresha shughuli zao.
“Tunalipa ushuru mara mbili kutoka kijijini hadi sokoni ukiachana na ushuru mdogomdogo unaotozwa ndani ya soko.”amesema Komba
Naye, Mkulima Benae Lwosu ameshukuru kupanda kwa bei ya mahindi na ametoa wito kwa Serikali kuboresha bei ya mazao mengine kama vile soya na kuwepo kwa soko huria litakalomruhusu mkulima kuuza soya mwenyewe.
Soko la SODECO linauza na kununua mazao mbalimbali kama vile Soya,mbaazi,mahindi na maharage.
Imeandaliwa na
Bacilius kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 6, 2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa