MBUNGE wa Jimbo la Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro anaèndelea na ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa Songea mjini kwa kumchagua kuwa Mbunge na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.
Tangu ameanza ziara Februari 23 hadi sasa katika kila kata anayotembelea anakutana na kilio cha mbolea kuuzwa kwa bei juu toka shilingi 41,000 iliyotangazwa awali hadi shilingi 60,000 hali ambayo imesababisha baadhi ya wakulima kushindwa kumudu kununua na hivi sasa mazao yao yameharibika kutokana na kukosa mbolea ambayo katika mkoa wa Ruvuma mbolea kwa mazao ni sawa na hewa ya Oksijeni kwa binadamu.
Imeandaliwa na Albano Midelo
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa