• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

POLISI JAMII MKOANI RUVUMA WAPEWA MAFUNZO KUBORESHA UTENDAJI KAZI

Tarehe ya kuwekwa: July 31st, 2023

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP  Gwisael Pagi amewataka Polisi Jamii Mkoani Ruvuma kufanya kazi kwa Weredi kwa kushirikiana na Wananchi ili kufichua na kudhibiti matukio ya kiuharifu katika jamii.

Hayo yamejiri katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Polisi jamii Mkoani Ruvuma yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 31 Julai 2023 yaliyoshirikisha Jeshi la Polisi, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kimila, pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kwa lengo la kutoa elimu ya ushirikishwaji katika masuala ya ulinzi shirikishi jamii.

ACP Pagi alisema mwaka 2006  kupitia waraka namba 3 wa Inspekta Jeneral wa Polisi  nchini umeweka msisitizo katika suala la Polisi Jamii huku wakitambua kwamba Sheria za Polis zinazungumzia Ushirikiano baina ya polisi  na jamii.

Alisema lengo la kukutana katika ukumbi huo ni kutekeleza mradi wa ukaguzi   na Polisi  kata katika kuzuia Uharifu ukiwa na malengo mahususi ya kusogeza huduma karibu na jamii ambao ulizinduliwa rasmi  na Kamishina wa Polisi Faustin Chinogile mnamo tarehe 24 julai 2003 Mkoani Lindi kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa  wa polis jamii nchini, ngazi ya Mkoa, Wilaya, na polisi kata pamoja na polisi  jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia, ubakaji, Migogoro ya ardhi, Ushoga na matukio ya uharifu.

Akizungumza Msatahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema anaishukuru Serikali katika kusimamia suala la ulinzi shirikishi wameweza kupeleka Polisi kata kila kata ili kulinda usalama wa Raia na mali zao “alipongeza”

Mhe. Mbano alisema Kwa upande wa Manispaa ya Songea suala la ulinzi shirikishi wamelipokea vizuri kwa kuwapokea Polisi kata kwa kila kata na kuwapa ushirikiano katika utendaji wa kazi zao za kila siku ikiwemo kutanzua baadhi ya changamoto ambazo hukwamisha utendaji wa kazi zao.

Ametoa rai kwa Serikali kuwawezesha Polisi kata kwa kuwapatia vitendea kazi kama Pikipiki ili kurahisisha utendaji wa kazi zao za kila siku ambapo pia amewataka Maafisa watendaji wa kata kutoa ushirikiano kwa Polisi kata hao kwa kuwsaidia  Pikipiki pale wanapohitaji usafiri wawapo kituoni hapo kwani hivi karibuni Maafisa Watendaji kata wanatarajia  kupewa Pikipiki kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi.


Kwa upande wake Kamisheni ya Polisi Jamii  kutoka makao Makuu Dkt. Ezekiel Kyogo SP alisema “ siku ya leo ni mwendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo askari kata pamoja na Viongozi wa Serikali za mitaa kwa lengo kwa kutoa elimu ya Farusafa ya jamii na ushiriki wa jamii katika mambo ya usalama pamoja na kupinga  ukatili wa kijinsia na kuwajenga polisi Kata waweze kuwa walimu katika jamii.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo walitoa shukrani kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataboresha utendaji wa kazi na kupunguza migogoro, na vitendo vya kikatili katika jamii .

Kauli mbiu;   “Polisi jamii kwa maendeleo ya jamii ”

 





Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI RUVUMA

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma Awapongeza Wastaafu 86 wa Kada ya Ualimu Mkoani Ruvuma

    May 08, 2025
  • Kamati ya Siasa Wilaya Yaridhishwa na Hatua za Miradi ya Maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

YALIYOJIRI MAKABIDHIANO YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa