SILAHA moja ya kivita aina ya AK 47,risasi sita na Meno mawili ya Tembo vimekamatwa katika kijiji cha Mangwamila kilichopo wilayani Songea kandokando ya mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Simon Marwa Maigwa akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake mjini Songea, amemtaja mtuhumiwa aitwaye Fidel Mangala Said ambaye aliweza kumtaja mtuhumiwa mwenzake aitwaye Maulid Japhary,miaka 45,mkazi wa kijiji cha Nambendo wilaya ya Songea ambaye awali alifanya jaribio la kutoroka na kukamatwa tarehe 15/7/2019.
Maigwa amesema meno hayo yenye thamani Zaidi ya milioni 34, waliyahifadhi kwenye mfuko wa Sulphate na kuyafukia ardhini shambani kwa mtuhumiwa Issa Musa Milanzi, Mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa Nambendo wilayani Songea wakiwa na mwenzake Fidelis Mangala,miaka 20 mkazi wa Nambendo.
“Watuhumiwa hao wamekiri kujihusisha kwa muda mrefu na uwindaji haramu na matukio mengine ya kihalifu ndani ya Tanzania na Nchi jirani ya Msumbiji”.amesema Maigwa.
Kamanda huyo wa polisi mkoani Ruvuma ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kukomesha vitendo vya kiharifu na waharifu.
Imeadaliwa na Farida Mussa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Julai 18,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa