JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kuua majambazi watano waliokuwa na siraha ya kivita yenye uwezo wa kupiga risasi 720 kwa dakika moja.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Mei 26 katika Mtaa wa Lusaka,Kata ya Bethelehem Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
“Majambazi hao waliuawa katika mapambano na Askari Polisi baada ya kugundua wanafuatiliwa’’,alisema.
Kamanda Maigwa amesema taarifa za awali zilionesha kuwa majambazi hao walikuwa wanaelekea eneo la machimbo ya dhahabu mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kufanya uharifu.
Amesema katika eneo hilo la tukio,kulipatikana silaha ya kivita aina ya medium machine Gun (MMG) ikiwa na mkanda wenye risasi 16 na bastola moja aina ya Glock ambazo zilikuwa zimebebwa na majambazi hao.
“Siraha hiyo yenye uwezo wa kupiga risasi 720 kwa dakika moja ni silaha hatari ya kivita iliyotengenezwa nchini Urusi mwaka 1969’’,alisisitiza Kamanda Maigwa.
Amesema jeshi la Polisi litaendelea kufanya misako endelevu kuhakikisha kuwa wanakamatwa wale wote wanaovunja sheria za nchi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Serikalini
Mei 27,2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa