Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Julai, 2018 amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa Mikoa, Wizara na Wilaya.Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho huo ili kujaza nafasi zilizo wazi kufuatia baadhi ya viongozi kustaafu, kuteuliwa katika nafasi nyingine na wengine kuachwa.Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo;
1. Bw. ALLY SALUM HAPI (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya AMINA MASENZA ambaye amestaafu.
2. Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU ambaye amestaafu.
3. Bw. ALBERT CHALAMILA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Anachukua nafasi ya Bw. AMOS GABRIEL MAKALA ambaye amehamishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu RAPHAEL MUHUGA amestaafu.
4. Brigedia Jenerali NICODEMAS ELIAS MWANGELA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Anachukua nafasi ya Luteni Mstaafu CHIKU GALLAWA ambaye amestaafu.Wakuu wa Mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa kama ifuatavyo:1. Bw. KESSY MADUKA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MADENGE2. Bw. ABOUBAKAR MUSSA KUNENGE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Bibi THERESIA MMBANDO.3. Bw. DAVID KAFULILA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.4. Bw. DENIS BANDISA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Anachukua nafasi ya SELESTINE GESIMBA5. Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Bibi. WAMOJA DICKOLAGWA.6. Bw. ABDALLAH MOHAMED MALELA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.7. Bw. RASHID KASSIM MCHATA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Anachukua nafasi ya Bw. CHARLES PALLANGYO.8. Bw. MISSAILE MUSSA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara. 9. Bi. CAROLINE ALBERT MTHAPULA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MARA.10. Dkt. JILLY ELIBARIKI MALEKO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi ya ALFRED LUANDA.11. Bw. CHRISTOPHER DEREK KADIO ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Mstaafu CLODWING MTWEVE.12. Bw. ERIC SHITINDI ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Anachukua nafasi ya BW. JACKSON SAITABAU.13. Prof. RIZIKI SALAS SHEMDOE ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Bw. HASSAN BENDEYEKO.Makatibu Tawala wa mikoa wafuatao wamehamishwa vituo vyao vya kazi.1. Bibi REHEMA MADENGE aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa DODOMA, amehamishiwa katika Mkoa wa Lindi.2. Bibi THERESIA MMBANDO aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa DAR ES SALAAM amehamishiwa katika Mkoa wa Pwani.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa