Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajia kuanza ziara ya kikazi kuanzia tarehe 20 Julai 2023 hadi 24 Julai 2023 Mkoani Ruvuma.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mkuu Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amesema “ tarehe 20 Julai 2023 Makamu wa Rais anatarajia kuwasili katika kijiji cha Lilondo Halmashauri ya Madaba na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali kisha atawasalimu wananchi, pia akiwa katika Halmashauri ya Madaba pia atawasalimia wananchi katika katika kijiji cha Mlilayoyo kisha kuondoka kuelekea Ikulu ndogo.
Alisema Tarehe 21 Julai 2023 atazindua kituo cha Afya Lilambo na kuongea na wananchi, kisha ataondoka kuelekea kijiji cha Matomondo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambako ataweka jiwe la msingi Barabara ya Kiwango cha Lami ya Matomondo hadi Mlale JKT yenye Urefu wa Km 4.5, pia ataongea na wananchi na kuelekea Peramiho ambapo atafungua Jengo la kusafisha Figo , na kukagua jengo la upasuaji pia na kusalimiana na wananchi.
Kanal Laban aliongeza kuwa Ziara hiyo itaendelea hadi tarehe 22 Julai ambapo atashiriki kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ( Mama Samia Legal Aid Campaign) itakayofanyika katika uwanja wa Majimaji.
Makamu wa Rais ataendelea na Ziara hadi tarehe 23 Julai ambapo atatembelea Wilaya ya Nyasa na Mbinga, na anatarajia kukamilisha ziara yake tarehe 24 Julai 2023 siku ya Jumatatu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa