MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kukagua miradi ya Mwenge wa Uhuru katika Halmashauuri ya Manispaa ya Songea.
Mndeme amekagua miradi mbalimbali inayakadiriwa kuwa na thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni moja ambayo inatarajiwa kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa Juni 7 mwaka huu ambapo Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa Manispaa ya Songea.
Mara baada ya kukagua miradi hiyo Kamati ya ulinzi na Usalama imeridhishwa na miradi hiyo,hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameagiza miradi ambayo bado haijakamilika kwa asilimia 100,ikamilishwa haraka.
Miradi ambayo imekaguliwa na Kamati hiyo ni mradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe uliopo Kata ya Lilambo wenye thamani ya shilingi milioni 10 na mradi wa ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Kiburang’oma wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 32.
Miradi mingine ni kiwanda cha kukoboa mpunga uliopo Kata ya Misufini wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 142,ujenzi wa zahanati ya St.Benjamini uliopo katika Kata ya Msamala wenye thamani ya shilingi milioni 468 na mradi wa maji Mitendewawa uliopo katika Kata ya Mshangano wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 517.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma pia imekagua miradi ya mapambano dhidi ya malaria katika shule ya msingi Chandarua wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni nane,mradi wa mabwawa ya samaki na utalii Kata ya Msamala wenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 71,Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kata ya Mjimwema wenye thamani ya Zaidi ya milioni 40 na mradi wa uwezeshaji vikundi vya wanawake na vijana uliogharimu milioni 20.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Mei 15,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa