MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa maagizo mazito ya kuhakikisha Halmashauri zote zinakusanya mapato kwa asilimia 100 na kwamba Halmashauri ambayo itashindwa kufikia malengo atashauri ifutwe au kushushwa daraja.
Mndeme alikuwa anazungumza na watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma mara baada ya kumuapisha Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo katika sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma mjini Songea.Sherehe hizo zimehudhuria na viongozi mbalimbali katika ngazi za wilaya na mkoa wakiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri,wakuu wa Taasisi na mashirika ya serikali,viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Ruvuma wakiwemo wanahabari.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa