Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amefanya ziara ya kuwatembelea Wamachinga katika soko la Mitumba lililopo kata ya Majengo kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara hao.
Ziara hiyo imefanyika kwa nyakati tofauti na kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee, viongozi wa dini, wafanyabiashara, bodaboda na bajaji, pamoja na wamachinga iliyofanyika tarehe 29 hadi tarehe 31 Januari 2024 ambayo ilishirikisha wakuu wa idara mbalimbali, taasis za kifedha, SOUWASA, TANESCO na wadau wengineo.
Akijijibu hoja hizo kutoka wamachinga ambapo amezitaka Taasis za kifedha hususani NMB kutoa mikopo kwa wajasiliamali bila usumbufu wowote ambao hupelekea wajasiliamali hao kushindwa kufanikisha kupata mkopo sambamba na kuwapa elimu ya ujasiliamali kwa wale watakaokuwa wamekidhi vigezo bila ya kuwapotezea muda wao.
Kanal Labani ameitaka Halmashauri Manispaa ya Songea kuhakikisha inasimamia swala la usafi wa mazingira, kuboresha miundombinu ya soko la majengo ikiwemo na ujenzi wa vyoo, pamoja na kuwapanga wamachinga kwenye maeneo yaliyo rasmi ifikapo tarehe 02 Februali 2024 iwe imetekelezwa.
Imeandaliwa na,
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa