Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. ahmed abbas ahmed amewataka viongozi wa Mkoa Ruvuma kuenfdelea kujipanga vizuri katika kuandaa tamasha la la 3 la utamaduni la kitaifa litakalofanyika mkoani Ruvuma.
Ameyasema hayo wakati wa kikao na viongozi mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambapo amesema kuwa, viongozi wanatakiwa kujiandaa vizuri kuptia tamasha hilo ili liweze kufanyika kwa ufasaha bila kujitokeza kwa changamoto zozote.
Aidha kupitia kikao hicho amewahimiza viongozi hao kuweza kuwahamsisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kupigia kura na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mtaa hapo Novemba mwaka huu.
Kanal. Ahmed amewasistizia viongozi hao kuendelea kuwakumbusha wananchi kuendelea kuandaa lishe bora ili kutokomeza tatizo la udumavu katika mkoani Ruvuma.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 05 Septemba 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea, ambacho kilihuidhuriwa na madiwani wote, viongozi ngazi ya wilaya, vyama vya siasa wataalamu pamoja na wadau mbalimbali kutoka halimashauri zote za mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kufanya maandalizi ya Tamasha la utamaduni kitafa, pamoja Kujadili na kuwasilisha taarifa kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika mnamo tarehe 27 Novemba mwaka huu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa