Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban.Thomas amekemea vikali ndoa ya jinsia moja kwa vijana ambayo ni uvunjifu wa Mila na Desturi za Afrika.
Amewataka Wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kupata mafanikio na kwa kupitia Elimu watakayoipata itawasaidia kusimamia Muungano na kutambua faida au manufaa ya Muungano.
Hayo yamejili wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao uliadhimishwa kwa kufanya ziara ya kutembelea miradi maendeleo na kuweka jiwe la Msingi la ufunguzi wa madarasa mawili ya awali yaliyojengwa kwa thamani ya shilingi Mil.43,160,000 fedha kutoka mfuko wa LANES 2021/202, uzinduzi wa Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Chabruma iliyojengwa kwa thamani ya Milioni 110 fedha kutoka Serikali kuu pamoja na upandaji wa miti kwenye maeneo ya shule kwa lengo la kuenzi Muungano wetu.
Kanal. Laban ametoa rai kwa wanachi wote kupanda miti ya vivuli, matunda kwa lengo la kulinda na kutunza mazingira ili yaweze kuboresha uoto wa asili na kuimarisha vyanzo vya maji.
Naye Afisa Misitu Manispaa ya Songea Godfrey Luhimbo alisema Manispaa ya Songea inaendelea na mkakati wa kupanda miti kila ambapo kupitia siku ya maadhimisho ya sherehe ya Muungano ilipandwa miche 3000 na kufanya jumla ya miche yote ambayo imepandwa katika msimu wa mwaka 2023 ni miche Mil.1,134,512. Alibainisha.
Kwa upande wa wanafunzi kutoka shule tofauti zilizotembelewa na Kiongozi huyo walitoa shukrani zao kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuwawezesha kupata miundombinu ya bora ya elimu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa