NAIPONGEZA Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kufaulisha kwa asilimia 85.51. Aidha, halmashauri ya Wilaya ya Songea inatakiwa kuongeza juhudi ili kupandisha ufaulu zaidi kwani matokeo yanaonesha wamefaulisha kwa asilimia 66.68.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa Wa Ruvuma Christina Mndeme akiwa katika kikao cha kamati ya Ushauri Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika tarehe 12 januari 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mndeme alianza kutoa shukrani kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwaletea maendeleo Watanzania wote, na Hii imejidhihirisha wakati wa maandalizi ya Uchaguzi na Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa kuhakikisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kinashinda kwa asilimia 84.1 kwa nafasi ya Rais, asilimia 78.2 kwa nafasi ya Ubunge na kufanya Majimbo yote tisa (9) kuwa miongoni mwa CCM na Kata 170 sawa na asilia 98.3. Ama hakika Ushindi huu ni mkubwa mno na haijawahi kutokea toka mfumo wa vyama vingi uanze “Hongereni sana!!.”
Akizungumzia kuhusu Elimu alisema matokeo ya kidato cha sita mwaka 2020, Mkoa umefanya vizuri kwa ufaulu wa asilimia 98.8. Miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2021, Takwimu zinaonesha hadi kufikia Novemba, 2020 kulikuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 43 kwa ajili ya kidato cha kwanza 2021. Ameagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaanza masomo Januari, 2021 na hakuna mtoto atakaebaki nyumbani kwa kukosa nafasi.
Aliongeza kuwa Mkoa wetu unatekeleza kampeni ya Magauni manne chini ya Kaulimbiu ya “Niache Nisome” ambapo Serikali ya Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu inapambana na kuhakikisha inaondoa na kumaliza vikwazo vinavyosababisha wanafunzi wa kike kushindwa kuhudhuria na kudumu shuleni ikiwemo kushindwa kumaliza masomo kutokana na mimba za utotoni. “ Alisisistiza”.
Alisema Katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 umelenga kulima hekta 672,137 za mazao ya chakula, Biashara na mazao ya bustani na kutarajia kuvuna tani 1,790,582, ambapo Mafanikio ya uzalishaji katika kilimo yanatokana na matumizi bora ya pembejeo za kilimo. Alibainisha kuwa, Serikali katika msimu huu 2020/2021 itaendelea na mfumo wa bei elekezi kununua pembejeo za kilimo hususan mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA). Pia Wizara ya kilimo pamoja na mamlaka ya udhibitii wa ubora wa mbolea Tanzania (TFRA) imetoa bei elekezi kwa kila Wilaya hapa Mkoani Ruvuma.
Aidha, Mkoa unaendelea kushirikiana na taasisi zingine za Serikali katika kusimamia zoezi la ununuzi wa Korosho kutoka kwa wakulima. Hadi sasa jumla ya kilo 14,826,644 za ya Korosho zenye thamani ya Tshs 33,893,774,357.00 zimeuzwa na minada inaendelea.
Akiipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kukusanya Mapato ya Ndani kwa 121.87% pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Songea tangu imeanza kutumia stendi kuu ya Shule ya Tanga tarehe 01 Januari, 2021 imeongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani yatokanayo na ushuru wa stendi na choo kutoka Tshs. 400,000 hadi Tshs. 900,000 kwa kila siku, kwa mwezi tunategemea Manispaa itakusanya zaidi ya Tshs. 27,000,000/=.
Alisema TRA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kukusanya Mapato ndani ya Mkoa mwaka 2019/2020, tumeweza kukusanya Tshs. 15,885,857,987.22 sawa na 94% na kwa kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021, TRA imekusanya jumla ya Tshs. 16,365,091,735.82 ambayo ni sawa na 105%. Hongereni sana.
Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Ruvuma Jairy Khanga akitoa ufafanuzi juu ya CHF iliyoboreshwa ambapo alisema CHF iliyoboreshwa ilianzishwa mwezi septemba mwaka 2019 hadi kufikia disemba 2019 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa umesajili kaya 2500, na hadi kufikia 2020 disemba Mkoa wa Ruvuma umesajili kaya 11,295 kukiwa na asilimia 10.5, kwa hiyo ili suala hili liweze kutekelezwa kwa ufasaha inabidi itolewe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu CHF iliyoboreshwa.
Khanga alisema ni Wilaya ya Tunduru katika kituo cha Matemanga pekee wamejitahidi kudai tofauti na vituo vingine hushindwa kudai madai kwa wakati.na kupelekea kukosekana kwa baadhi ya huduma za afya.
Amezitaka Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kuwaagiza waganga wakuu wa kila Halmashauri kuhakikisha wanawaandika barua kwa wasimamizi wa kila kituo cha Zahanati/Kituo cha Afya kwaajili ya kuwahimiza kuandika barua za madai (CHF) ili kuboresha huduma za kwenye vituo vya afya.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
13 Januari 2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa