MKOA wa Ruvuma unakabiliwa na upungufu mkubwa wa wauguzi hali ambayo inasababisha baadhi ya wauguzi waliopo kufanya kazi kwa saa 12 badala ya saa nane ambazo zinakubalika kisheria.
Akisoma risala ya Chama cha Waaguzi Tanzania cha Mkoa wa Ruvuma (TANNA) kwenye mkutano wa siku tatu ambao unafanyika kwenye ukumbi wa Songea klabu,Katibu Mwenezi wa TANNA Mkoa wa Ruvuma Oraph Pili amesema takwimu za Juni 2017 zinaonesha kuwa mkoa wa Ruvuma una asilimia 35 tu ya wauguzi zaidi ya 3000 wanaotakiwa ambapo upungufu wa wauguzi ni asilimia 65.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewapongeza wauguzi kwa kuendelea kufanyakazi kwa weledi licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi ambapo ameahidi serikali itazifanyia kazi changamoto zote ambazo wamezitaja katika risala yao.
Chama cha Wauguzi katika Mkoa wa Ruvuma kinaundwa na jumla ya matawi kumi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ya chama hicho ni Wauguzi Nguzo ya kuyafikia malengo Endelevu ya Maendeleo.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa