MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassan Mshaweji amezitaja sababu za wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga kuondolewa barabarani na kuwapeleka katika maeneo maalum yaliotengwa kwa ajili yao ni kuhakikisha wanafanya biashara katika maeneo salama na kuondoka barabarani ambako ni maeneo hatarishi.
" usalama wa wananchi ni kuhakikisha wanafanyakazi katika maeneo salama hivyo wamachinga tumewaandalia eneo la Majengo ambako tunatengeneza barabara kwa kiwango hiyo katika kiwango cha lami,tunatarajia hadi Novemba itakamilika,tunaweka taa barabarani na miundombinu ya vyoo na maji hivyo watakuwa huru kufanya biashara zao badala ya barabarani ambako ni hatari kwa usalama wao'',anasisitiza Mshaweji.
Amesema Manispaa ya Songea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walifanya zoezi la kuwaondoa wamachinga katika maeneo ya barabarani na kwamba zoezi hilo ni endelevu kwa kuwa Manispaa itaendelea kuwaondoa wamachinga watakaopanga bidhaa barabarani kwa usalama wao na ametoa rai kwa wafanyabiashara hao watii sheria bila shuruti.
Uchunguzi umeonesha baadhi ya maeneo machache ambayo sio barabara kuu baadhi ya wamachinga wameonekana wanapanga biashara zao,hata hivyo idadi kubwa ya wamachinga wametii agizo la serikali kuondoka barabarani na kwenda katika maeneo rasmi ambayo wameandaliwa ba Manispaa ya Songea ili waweze kufanyabiashara zao kwa amani na utulivu.
Hata hivyo Mstahiki Meya amewasisitizia wafanyabiashara wachache ambao bado hawajaenda katika eneo la Majengo watoke barabarani na kwenda kuungana na wenzao kufanyabiashara na kwamba waache kisingizio kuwa katika eneo la Majengo halifai kwa biashara jambo ambalo sio sahihi kwa sababu wenzao wanafanyabiashara na kupata faida katika maeneo hayo.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 17,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa