Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Jumbe Mwenye katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiliamali ya umuhimu na matumizi ya Msimbomilia (BARCODES), Mfumo Wa ufuatiliki (TRACEABILITY), viwango, Usajili wa Makampuni, umuhimu wa kulipa Kodi, Masoko na Viwanda iliyofanyika 04/02/2020 katika ukumbi wa familia takatifu kata ya Bombambili Manispaa ya Songea.
Mgeni Rasmi katika mafuzo hayo alikuwa Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassan Mshaweji . Ambapo katika hotuba yake aliyoisoma katika ufunguzi wa mafunzo hayo alisema, “GS1 ni Asasi isiyotengeneza faida (Not for Profit) ambayo imejikita katika kujenga na kusimamia Ubora wa Bidhaa kitaifa na kimataifa na kuainisha sababu ambazo zinatumika kuimarisha ushindani na muonekano mzima wa mnyororo wa msambazaji kutoka kwa mzalishaji mmoja mpaka makampuni makubwa na kufuatilia bidhaa hiyo hadi mlaji wa mwisho”.
Mshaweji alisema, BARCODES ni alama za utambuzi wa Bidhaa ambazo zinatoa maelezo ya Bidhaa husika zikisomwa na Mashine maalumu.
Alizijtaja faida za kutumia BARCODES ni pamoja na; bidhaa ya Tanzania kukubalika masoko ya ndani na nje ya nchi, kuongeza mauzo ya bidhaa zilizotayari badala ya kuuza mali gafi, kurasimisha wafanyabiashara, ukusanyaji wa kodi kwa kusajili walipa kodi wapya, na ukusanyaji wa takwimu, kuongeza ajira kwa vijana, kutanua wigo, usahihi wa bei.
Naye Afisa masoko GS1 Tanzania Erick Kafula alibainisha kuwa, Nanukuu “ Namba zote zinatambuliwa na kiambishi awali cha nchi husika mfano; Kenya 616, South Africa 600, United Kingdom 500, China 690, Tanzania 620, kwa mfano wa BARCODE/ MSIMBOMILIA , 620 hutambulisha Nchi ya Tanzania, 000000 GS1 Code ya kampuni, 000 namba ya bidhaa, 8 bei ya bidhaa.” Aliongeza kuwa ada ya usajili mwanachama 100,000/=, na ada ya uanachama 100,000 – 2,640,000/= inategemea na pato la mwaka la mjasiliamali/ kampuni. Hivyo aliwasihi wajasiliamali wa Songea kusajili biashara zao kwa kutumia msimbomilia ili waweze kupeleka biashara zao kwenye masoko makubwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa