PORI la Akiba la Selous lilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani likiwa pori la kwanza kutengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori barani Afrika na la pili kwa ukubwa duniani baada ya pori la Marekani ambalo linaitwa Yellowstone National Park.
Historia inaonesha kuwa jina la Selous limetokana na askari ambaye alikuwa ni mvumbuzi wa kiingereza aliyeitwa kapteni Fredrick Selous aliyefariki Januari 4, mwaka 1917 na kuzikwa katika eneo la Behobeho lililopo ndani ya pori la Selous .
Pori la Akiba Selous lina utajiri wa viumbe adimu katika sura ya dunia kama vile nyani aina ya sanje,mbega mwekundu,faru mweusi ambaye yupo hatarini kutoweka na wanyama wengine wakiwemo ndege,wadudu na mimea ambayo haipatikani sehemu nyingine yeyote duniani.
Kutokana na umuhimu wa pori la Selous Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Utamaduni na Sayansi (UNESCO) limelihorodhesha pori hilo kuwa ni moja ya maeneo ya asili ya urithi wa dunia tangu mwaka 1982.
Imeandaliwa na Albano Midelo
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa