WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema serikali kuanzia mwaka 2019 inatarahis kutoa dawa Mpya ya kufubaza virusi vya UKIMWI.Mwalimu amesema hayo wakati anazindua kampeni ya Furaha Yangu ngazi ya mkoa wa Ruvuma ndani ya uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Waziri Mwalimu amesema pia serikali inaanza kutoa dozi ya dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI ambazo mteja anazitumia kwa miezi mitatu badala ya mara moja kila mwezi na kwamba dawa hizo zitatolewa kwa wateja waaminifu na kwamba lengo ni kutoa dawa kwa mara moja ambazo mteja atazitumia kwa miezi sita ili kumpunguzia usumbufu wa kila mwezi kufuata dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa