SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imemtambua rasmi mzee Benedict Rasha(Local GPS) aliyegundua kuungua kwa rasilimali ya nchi Madini ya makaa ya mawe mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga mkoani Ruvuma mwaka 2006. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemkabidhi mzee huyo kiasi cha shilingi milioni 5,000,000 kutambua mchango wake katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na familia ya mzee Rasha,viongozi wa serikali ngazi ya wilaya ya Mbinga na mkoa,Watendaji wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya TANCOAL na wanahabari.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa