Tarehe 16 Septemba ni siku ya Usafi Duniani, katika kutekeleza maadhimisho haya, Wilaya ya Songea imefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya kijamii kwa nyakati tofauti ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Kwa upande wa Manispaa ya Songea maadhimisho hayo yamefanyika kwa kufanya usafi katika maeneo yote ya masoko, Taasisi pamoja na kila mwananchi kuhakikisha anafanya usafi kwenye kaya yake.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kukamilisha usafi wa mazingira , Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile amewataka viongozi ngazi ya kata na mitaa, pamoja na wananchi wote kuhakikisha usafi unafanyika ipasavyo kwa kushirikiana na wananchi ili mji uweze kuwa safi. “Alisisitiza”.
Ndile alisema” Usafi wa mazingira ni jambo mtambuka hivyo amewataka Halmashauri kuongeza jitihada za kuondoa taka katikati ya mji pamoja na kuongeza vitendea kazi vya usafi wa mazingira.”
Akiishukuru Menejiment ya WASAFI Media kwa kushiriki matukio ya usafi wa mazingira katika soko la Bombambili pamoja na kuendesha Kongamano la JIONGEZE ni jukumu lako ambalo limefanyika tarehe 15 Septemba 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kutoa elimu ya kufungua fursa za kiuchumi na uwekezaji Mkoani Ruvuma. “ Aliwashukuru"
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano, alisema ili kutatua changamoto za usafi wa mazingira, Manispaa ya Songea imeweka mpango mkakati wa kujenga Dampo, kuongeza vitendea kazi vya usafi, pamoja na kutumia kampuni kwa ajili ya kuzoa taka. “ Alibanisha’
“Mwisho”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa