Mkuu wa wilaya Mhe. Kapenjama Ndile amekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya na lishe pamoja na watendaji kata 17 Novemba 2025 katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa lengo la kujadili sababu za ongezeko kubwa la idadi ya watoto waliozaliwa na uzito pungufu wa kg2.5 katika Manispaa ya Songea.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Ndile alibainisha kuwa katika miaka miwili iliyopita 100% ya watoto 57 waliolengwa walikua wanapata chakula shuleni, hata hivyo hadi kufikia mwezi huu idadi ya watoto wanaopata chakula shuleni imefikia watoto 72. jambo ambalo linaonesha mafanikio ya jitihada za lishe shuleni.
Aidha alibainisha kuwa kwanzia mwezi Juni hadi septemba 2025 walizaliwa watoto 2528 na katika hao zaidi ya watoto 224 (sawa na 7%) walikuwa na uzito pungufu wa kg2.5
Ameeleza kuwa sababu kubwa ya changamoto hiyo ni hali duni ya lishe kwa wajawazito, mimba za ototoni pamoja na kifafa cha mimba. Aidha Alisisitiza kuwa kuna haja kubwa ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu afya ya mama na mtoto na kuwahimiza wajawazito kuhudhuria kliniki ili kupata ushauri stahiki kutoka kwa wahudumu wa afya.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa