NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
01.10.2021
“Stendi ya Mfaranyaki iendelee kutumika kwa ajili ya matumizi ya daladala zinazosafirisha abiria tu ndani ya Manispaa ya Songea”
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema hapo jana tarehe 30 Septemba 2021 wakati akiwasilisha makubaliano ya kikao kilichofanyika tarehe 29 Septemba 2021 kati ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Generali Wilbert Ibuge, viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea pamoja na viongozi wa umoja wa wasafirishaji abiria Ruvuma (UWARU).
Mgema alieleza kuwa kila mmiliki/ kampuni ya mabasi ya usafirishaji anatakiwa kuhakikisha ifikapo tarehe 30 Desemba 2021 iwe imehamishia shughuli zake za kukatia tiketi na mizigo katika stendi kuu ya Tanga na ofisi hizo ziwe zimehamishwa katika stendi ya Mfaranyaki.
Aliongeza kuwa mabasi yote ya Mikoani yakifika na abiria katika stendi kuu ya Tanga kuanzia muda wa saa 4:00 usiku, na endapo katika stendi hiyo hakuna daladala ya kuwasafirishia abiria kwa ajili ya kuwaleta katikati ya Mji, Mabasi yameruhusiwa kuwaleta abiria katika stendi ya Mfaranyaki na utaratibu huu ni kwa muda wa mpito wa miezi mitatu kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 30 Desemba 2021.
Mabasi yote ya abiria yanapoelekea stendi ya Tanga nyakati za asubuhi yameruhusiwa kuchukua abiria wenye tiketi katika stendi ya Mfaranyaki kuanzia muda wa saa 10:00 hadi 10:30 alfajiri na yanapoelekea stendi kuu ya Tanga yanaruhuwiwa kuchukua abiria kituo cha Bombambili, Msamala na mshangano, na ifikapo saa 10:31 Alfajiri mabasi yote hayaruhusiwi kuwepo katika stendi ya Mfaranyaki. “Mgema Alisisitiza”
Alihitimisha kwa kusema kuwa mabasi yote yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Lindi yataanza safari zake stendi kuu ya Tanga na yanaporudi yatashusha abiria katika kituo cha Seedfarm, endapo yatafika kuanzia saa 4:00 usiku na katika basi hilo kuna abiria wanaokwenda maeneo ya Bombambili, Msamala na Mshangano basi hilo litalazimika kumalizia safari yake katika stendi kuu ya Tanga.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa