• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAKUKURU Mkoani Ruvuma Yaokoa Fedha Zaidi ya Mil. 359 kuanzia Aprili hadi Juni 2020.

Tarehe ya kuwekwa: July 16th, 2020

Taasisi ya Kuzuwia na Kupambana na Rushwa Mkoani Ruvuma imewataka Wananchi kutoa ushirikiano katika kudhibiti vitendo vya rushwa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2020.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Owen Ajasson wakati akitoa taarifa ya Utendaji  kazi wa TAKUKURU kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2020 iliyofanyika katika  ofisi za  TAKUKURU Mkoa leo 16.07.2020.

Ajasson amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kutoa Ushirikiano wa kudhibiti vitendo vya Rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa vitakavyo fanywa na Wagombea mbalimbali kwa nafasi za  Udiwani na Ubunge pamoja na wapambe wao.

Ajasson alisema, nanukuu“TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma tumejipanga kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wagombea na kampeni zao na wapambe wao ili kuzuwia na kupambana na Rushwa” mwisho wa kunukuu.

Amesema Katika kipindi cha miezi mitatu Taasisi hiyo imefanikiwa kukokoa kiasi cha fedha zaidi ya  Sh. Milioni 359 kutoka vyama vya Ushirika (SACCOS), kwa Wilaya ya Songea, Mbinga, na Namtumbo, Makusanyo ya Vitambulisho ya wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) kwa Wilaya ya Tunduru, Mbinga, Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika kijiji cha Makwaya kata ya Muhukuru- Lilahi, na maeneo mengine ni Sekta ya Elimu, Benki ya Wananchi Mbinga, na Ubadhilifu wa Makusanyo yatokanayo na  POS pamoja na dhuluma dhidi ya wakulima wa zao la korosho.

Aliongeza kuwa katika kipindi tajwa Taasisi hiyo imefanya ufuatiliaji wa miradi  8 ya maendeleo  ambayo ni ujenzi wa Miundombinu na afya yenye zaidi ya thamani ya sh. bilioni moja na milioni mia nane miradi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea na maeneo mengine ikiwemo  ujenzi wa kituo cha afya Magagura na Matimila na matengenezo ya Barabara ya Maposeni hadi Likingo unaosimamiwa na TARURA.

Ajasson amesema Katika ukaguzi wa Miradi wa matengenezo ya Barabara ya Maposeni hadi Likingo Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilibainika kwamba alama za Barabarani katika barabara hiyo hazijawekwa na kipande cha kiliometa 3 ambacho kilitakiwa kiwekewe kifusi hakijawekewa.

TAKUKURU kwa kipindi cha Julai- Septemba imejipanga kuendelea kuelimisha wananchi kupiga vita vitendo dhidi ya  rushwa katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi oktoba 2020 ili wasikubali kurubuniwa kwa vitendo vya Rushwa na kutambua haki na wajibu wao wa kufahamu Uchaguzi ninini, lengo la Uchaguzi, sheria inayoongoza uchaguzi pamoja na umuhimu wa kupiga kura.

IMEANDALIWA NA;

AMINA PILLY,

16.07.2020

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa