TAKUKURU Mkoani Ruvuma imefanikiwa kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bil. 6 ambayo imekutwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo na miradi kutokamilika kwa wakati, ununuzi wa vifaa vichache, na ucheleweshaji wa malipo ya Mafundi.
Katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo, Miradi mitano yenye thamani ya shilingi 5,510,000,000 ilikuwa na mapungufu ikiwemo na mradi wa ujenzi wa Madaasa 9katika Shule ya Sekondari Sasawala Wilaya ya Namtumbo kwa thamani ya 180,000,000, Ujenzi wa majengo Matatu katika Hosptali ya Wilaya ya Namtumbo kwa thamani ya 800,000,000, jengo la wagonjwa wan je katika Hosptali ya Rufaa Mkoa Songea kwa thamani ya 3,870,000,000, ujenzi wa Hosptal ya Wilaya ya Mbinga 500,000,000 pamoja na kituo cha afya Mbangamao 250,000,000.
Hayo yamejili katika kikao cha Waandishi wa Habari kilichofanyika leo 18 Mei 2023 katika ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuuhabarisha umma kuhusu utendaji kazi wa ofisi ya TAKUKURU katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi januari hadi machi 2023.
Akitoa ufafanuzi Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule alisema “ Miongoni mwa mikakati itakayotekelezwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya Rushwa na madhara yake katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuendelea kufanya kazi za kuzuiia na kuchukua hatua kwa wale wote watakao kutwa na tuhuma za vitendo vya Rushwa ikiwa ni pamoja na kwafikisha Mahakamani, kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa watakao kutwa na tuhuma za vitendo vya Rushwa, na kushirikiana vijana wa Skauti katika kutoa elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa pamoja na Program Rafiki.
Janeth ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano na TAKUKURU kwa taarifa zenye kuashiria vitendo vya Rushwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa