TAKUKURU mkoani Ruvuma imeweza kufanya kazi za udhibiti katika mifumo ya utoaji huduma 20 katika idara zilizo lalamikiwa kwa nia ya kutafuta nia ya kutafuta namna ya kuziba mianya ya rushwa iliyopo.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yustina Chagaka akielezea utafiti na udhibiti wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha kuanzia Julai 2017 hadi Juni 2018 amesema TAKUKURU imefanya vikao vya wadau 10 kwa nia ya kujadili mianya ya rushwa na namna ya kufanya marekebisho ili kuondoa mianya hiyo.
Amezitaja sekta na Idara zilizofanyiwa udhibiti kuwa ni Maji,Ardhi, Ustawi wa jamii, ya Afya, Mazingira, Mahakama,maliasili,uvuvi na Usalama barabarani katika wilaya za Songea,Mbinga,Namtumbo na Tunduru.
Idara nyingine amezitaja kuwa ni Elimu,Afya,ukusanyaji wa mapato na Ushirika katika Halmashauri za Namtumbo,Songea,Tunduru na Mbinga.
“TAKUKURU Ruvuma imefanya kazi za ufuatiliaji wa utekelezaji wa maazimio yaliowekwa na wadau kwenye warsha tisa katika sekta ya Elimu, ukaguzi na uteketezaji wa bidhaa bandia, zilizopitwa na wakati na zenye sumu’’,anasisitiza Yustina Chagaka.
TAKUKURU Ruvuma inaendelea kuwaasa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano haya kwa kukataa kujihusisha na vitendo vya rushwa, kukemea na kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika ofisi za TAKUKURU zilizopo katika kila Wilaya au kwa viongozi mbalimbali wa Serikali.
Imetolewa na,
Victoria Ndejembi,
Kitengo TEHAMA Manispaa Songea
Agosti 9,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa