• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAKUKURU Ruvuma Yaokoa Mamilioni ya Fedha.

Tarehe ya kuwekwa: April 29th, 2021

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Ruvuma imeokoa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 102,968,122/= ambazo zimepatikana baada ya chunguzi mbalimbali kufanyika.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Owen Jasson, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Marchi 2021 kwa Waandishi wa Habari iliyofanyika  katika ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma tarehe 28 Aprili 2021.

Jasson alisema katika kipindi cha miezi mitatu, Taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa fedha kiasi cha jumla ya Shilingi Milioni 102,968,122/= ambayo imeokolewa kutokana na chunguzi zilizofanyika kwenye vyama vya ushirika (SACCOS)  Wilaya ya Songea, Mbinga, Namtumbo, Tunduru na Nyasa.

Jasson alibainisha kuwa  fedha hizo zimetokana na marejesho ya madeni kutoka kwenye vyama mbalimbali vya ushirika katika mkoa wa Ruvuma ikiwemo na SACCOS ya walimu (Tunduru), Nambawala AMCOS (Nyasa), Kurugenzi SACCOS (Mbinga), SACCOS (Songea) pamoja na Libango AMCOS (Namtumbo).

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho tajwa, Taasisi hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 13 Mkoa wa Ruvuma ambayo ni ujenzi wa miundo mbinu ya maji, barabara, elimu na huduma za vikundi, inayotekelezwa katika Wilaya zote Mkoani Ruvuma  yenye thamani Zaidi ya Shilingi Bilioni moja ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba 7 za watumishi wa Wilaya ya Madaba.

Aliongeza kuwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kufanya semina na mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali kwa ajili ya  kutoa elimu kwa jamii juu ya mapambano dhidi ya Rushwa, na kuimarisha klabu za wapinga Rushwa katika shule za msingi na sekondari, Jasson ‘Alisema’.

Aidha, amewashukuru Wananchi kwa kusaidia Taasisi hiyo katika kutoa taarifa kuhusiana na vitendo vya Rushwa kupitia vyanzo mbalimbali ambapo wamefanikisha kupokelewa kwa taarifa 133 katika kipindi hicho cha Januari hadi Marchi 2021.

TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imejipanga kuendelea kuelimisha jamii kupiga vita Rushwa kwa kuwafahamisha madhara ya kutoa na kupokea Rushwa, kutoa taarifa mapema juu ya vitendo vya Rushwa, kuwa tayari kutoa ushahidi pale inapohitajika pamoja na kuendelea kufuatilia miradi ya maendeleo linayoendelea kutekelezwa katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2021.

IMEANDALIWA NA,

AMINA PILLY,

AFISA HABARI MANISPAA,

28.04.2021.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa