WAWAKILISHI kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Makao makuu ya nchi jijini Dodoma,wametembelea na kukagua mradi wa kituo cha Afya Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Wawakilishi hao wakiongozwa na Khalifa Kondo wameridhishwa na ujenzi huo ambao umefikia zaidi ya asilimia 98 ukiwa umegharimu shilingi milioni 400.Kituo hicho kina majengo manne ambayo ni jengo la wagonjwa wa nje,upasuajii,mama na mtoto na maabara.Kituo hicho baada ya kukamilika kinatarajia kuhudumia wakazi 45,000 kutoka katika kata tano
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa