TAMISEMI YATOA MAFUNZO kwa KAMATI ZA MALALAMIKO
WIZARA ya Tawala za Mikoa na Serikali za MitaaTAMISEMI katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetoa elimu kwa kamati za malalamiko za kata kuhusu Urban Local Government Strengtherning Program(ULGSP) katika Manispaa hiyo .
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo,wajumbe,wawakilishi wa kamati za malalamiko kutoka katika kata 21 zilizopo katika Manispaa hiyo na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Songea.
Mwakilishi wa TAMISEMI akizungumza katika mafunzo hayo ya siku moja amewaasa wanakamati hao kuelimisha wananchi kuhusu miradi ya ULGSP kuwa ni miradi ya Serikali na sio miradi ya Benki ya Dunia.
Hata hivyo amesema Benki ya Dunia hufuatilia na kukagua matumizi ya fedha, miradi na mahusiano katika Halmashauri husika ili kuhakikisha miradi inakuwa na tija na ufanisi.
“Lengo la ULGSP ni kuboresha miundo mbinu, kuongeza usalama wa makazi, kuongeza thamani ya makazi na pia kuongeza kipato cha wananchi, Halmashauri na Taifa’’,alisisitiza Mwakilishi wa TAMISEMI
TAMISEMI imewakumbusha wanakamati kuendelea kupokea malalamiko na kujadili migogoro yote kuhusu ULGSP na kuipatia ufumbuzi kwa muda muafaka pia wahakikishe wananchi wanafahamu uwepo wa kamati hizo.
Imetolewa na,
Victoria Ndejembi
Kitengo TEHAMA Manispaa Songea,
Agosti,13,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa