Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Songea Mjini kwa kuzingatia kanuni ya 14 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za Mwaka 2020 na kanuni ya 12 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2020, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za Watendaji wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 kama ifuatavyo:-
Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi;
Asiwe shabiki au kiongozi wa chama cha siasa;
Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu;
Awe amemaliza elimu ya kidato cha nne (4) au zaidi na anaweza kusoma na kuandika vizuri. Pia, anayeweza kuyaelewa Maelekezo ya Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura; na
Ikiwezekana awe mkazi wa kata ambayo anaomba.
Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi;
Awe mkazi wa kata ambayo atafanyia kazi ya kuongoza wapiga kura;
Ikiwezekana awe mpiga kura wa kituo anachofanyia kazi;
Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu;
Awe na elimu isiyopungua kidato cha nne na anayeweza kusoma na kuyaelewa Maelekezo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura; na
Asiwe shabiki au kiongozi wa chama cha siasa.
Malipo yatakuwa kama ifuatavyo:-
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
JIMBO LA SONGEA MJINI
21.09.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa