MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA ANAUZA VIWANJA VILIVYOPIMWA KATIKA ENEO LA LILAMBO KWA AJILI YA MATUMIZI YA VIWANDA VIDOGO, MAKAZI NA BIASHARA NA HUDUMA ZOTE ZA KIJAMII.
VIWANJA HIVYO VIPO PEMBEZONI NA BARABARA YA SONGEA, NA MIUNDOMBINU WEZESHI KAMA ( MAJI, BARABARA NA UMEME) IPO KWENYE ENEO LA MRADI.
AIDHA, BARABARA ZOTE ZA NDANI ZA MRADI ZIMECHONGWA NA ZINAPITIKA WAKATI WOTE. BEI YA VIWANJA HIVYO TSH 2000/= KWA MITA MOJAMOJA YA MRABA.
FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA KATIKA OFISI YA IDARA YA ARDHI NA MIPANGO YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA. BEI YA FOMU MOJA NI SH 20,000/= KWA KILA FOMU MOJA AMBAYO HAZITA RUDISHA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA;
MKURUGENZI MANISPAA
12. 11.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa