MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WAMILIKI WOTE WA VIWANJA NA MASHAMBA YALIYOKO NDANI YA MANISPAA YA SONGEA, KUWA WANATAKIWA KULIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KWA VIWANJA NA MASHAMBA WANAYOMILIKI, KABLA YA TAREHE 30.12.2020, ILI KUEPUSHA ADHABU ZITAKAZOANZA KUTOLEWA KUANZIA 01.01.2021.
BAADA YA MUDA HUO KUPITA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YA WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARHI, IKIWEMO KUNYANG’ANYWA NA KUUZA KIWANJA/ SHAMBA, AU KUSHIKA MALI YA MDAIWA ILI KULIPA DENI LA SERIKALI.
MAJINA YA WASIOLIPA KODI YAPO KWENYE OFISI YA KILA KATA. PIA WADAIWA WOTE SUGU WANAODAIWA KODI YA ARDHI, KUANZIA TSH 200,000/= WAMEANZA KUCHUKULIWA ZA KISHERIA.
PIA NI MARUFUKUM KUFANYA UJENZI WOWOTE BILA KIBALI CHA UJENZI, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO, IKIWA NI PAMOJA NA KUTOZWA FAINI AU KUVUNJIWA KWA JENGO HUSIKA.
NA WALE WOTE WENYE VIBALI VYA UJENZI WAACHE NAKALA ZA VIBALI VYA UJENZI KWA MAFUNDI WANAOENDELEA NA UJENZI.
IMETOLEWA NA;
MKURUGENZI MANISPAA YA SONGEA;
12.11.2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa