(LINARUDIWA)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea anawatangazia wananchi wote wenye sifa na nia ya kufanyakazi ya muda (Mkataba) kwa nafasi zifuatazo:-
1. DEREVA WA MITAMBO – NAFASI 01
a) Sifa za Mwombaji;
Awe mwenye umri kati ya miaka 18 hadi miaka 45.
b) Kazi za Kufanya;
Kuendesha Mitambo chini ya usimamizi wa Dereva mitambo mwenye uzoefu;
2. MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 01
a) Sifa za Mwombaji;
Awe na elimu ya kidato cha nne;
Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA.
Awe mwenye umri kati ya miaka 18 hadi miaka 45.
b) Kazi za Kufanya;
Kuandika na kutunza “Register” zinazohusu shughuli za uhasibu;
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha;
Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu;
Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki;
Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa, Barabara ya Sokoine, S.L .P 14, Songea. Simu:0252602970,
Nukushi: 0252602474, Barua pepe: md@songeamc.go.tz, Tovuti: www.songeamc.go.tz
3. MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (DAWA) - NAFASI 02
a) Sifa za Mwombaji;
Awe na elimu ya kidato cha nne;
Awe na cheti cha miaka miwili katika fani ya Mtekonolojia (Dawa) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na mabaraza yao pale inapohusika.
Awe mwenye umri kati ya miaka 18 hadi miaka 45.
b) Kazi za Kufanya;
Kuandaa mahitaji na matumizi ya dawa na vifaa tiba;
Kuagiza, kuhifadhi na kugawa dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi;
Kuandaa taarifa ya matumizi ya dawa na vifaa tiba;
Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba;
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4. MAELEZO YA JUMLA KWA KAZI ZOTE;
Kazi hizi ni za masharti ya muda (Mkataba);
Mshahara wa kazi hizi utazingatia viwango vya Mishahara Serikalini.
Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu, taaluma, cheti cha kuzaliwa na picha mbili (Passport size);
Mwombaji awe hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai au kuachishwa kazi serikalini kwa makosa ya utovu wa nidhamu;
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 23/03/2021 saa 9.30 alasiri;
Waombaji walioleta maombi ya tangazo la awali hawatahitajika kuomba tena;
Maombi yatumwe au kuletwa kwa:-
MKURUGENZI WA MANISPAA,
MANISPAA YA SONGEA,
S. L. P 14,
SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa