Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea anapenda kuwatangazia wananchi wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi ya Ajira ya Muda (Vibarua) kwa nafasi ya Wakusanya Ushuru - Nafasi 62.
Awe Mtanzania Mkazi wa Manispaa ya Songea.
Awe na Umri sio chini ya Miaka 18 na sio zaidi ya Miaka 55.
Awe na Elimu ya Darasa la Saba na Kuendelea.
Awe Muadilifu, Mwaminifu na hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
Awe uzoefu wa kutumia “Smart-Phone” katika miamala ya malipo.
2. KAZI/MAJUKUMU;
Kukusanya Ushuru wa Stendi,Vyoo, Mazao ya Chakula/Misitu, Maegesho na/au kadri atakavyopangiwa na Afisa Mapato.
3.MASHARTI YA JUMLA;
Barua ya maombi iambatanishwe na cheti cha kuzaliwa, picha moja ‘Passport size’ , barua ya Mdhamini mwenye mali isiyohamishika ndani ya Manispaa ya Songea na Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa/Mtendaji wa Mtaa anaoishi Mdhamini na Mwombaji wa kazi.
Kazi hii ni ya Mkataba wa Miezi Mitatu ambayo Malipo yake yatatokana na Asilimia ya Makusanyo .
Barua za maombi ziletwe kwa mkono ifikapo au kabla ya tarehe 23/03/2020 kwa anuani ya:-
Mkurugenzi wa Manispaa,
Manispaa ya Songea,
S. L. P 14,
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa