|
NAMBA YA ZABUNI: LGA/103/2021/2022/NCS/46 LOT 2
ZABUNI YA KUFANYA USAFI ,KUKUSANYA TAKA NGUMU KWENYE MAKAZI YA WATU ,MAJENGO YA BIASHARA,MASOKO,STENDI ZA MABASI,MITAA NA OFISI MBALIMBALI KUZOA TAKA NA KUZIPELEKA DAMPO LA SUBIRA NA KUKUSANYA ADA ZA TAKA KATIKA KAYA ZOTE KATA ZA MISUFINI,MATARAWE NA BOMBAMBILI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
S.L.P 14
May, 2022
YALIYOMO
SEHEMU YA KWANZA: MWALIKO WA ZABUNI 1
SEHEMUYA PILI: MAELEKEZO KWA WAZABUNI 3
SEHEMU YA TATU: LOHODATA YA ZABUNI (LDZ) 11
SEHEMU YA NNE; JEDWALI LA MAHITAJI NA BEI 14
SEHEMU YA TANO: MAELEZO YA VIGEZO MSAWAZO VYA KIUFUNDI 15
SEHEMU YA SITA: AGIZO LA UNUNUZI (ALU) 16
VIGEZO NA MASHARTI YA AGIZO LA UNUNUZI: 18
SEHEMU YA SABA: MASHARTI YA JUMLA YA MKATABA (MJM) 21
SEHEMU YA NANE: MASHARTI MAALUM YA MKATABA (MMM) AU AGIZO LA UNUNUZI (ALU) 39
MASHARTI MAALUM YA MKATABA.. 40
AHADI YA MTOA HUDUMA KUHUSU SERA DHIDI YA RUSHWA, KANUNI ZA MAADILINA PROGRAMU YA UKIDHI 53
ALU - Agizo la Ununuzi.
MJM - Masharti ya Jumla ya Mkataba
MMM - Masharti Maalum ya Mkataba
MZ - Mwaliko wa Zabuni
NSZ - Nyaraka Sanifu za Mwaliko wa Zabuni
PPA - Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410
TANePS - Mfumo wa Kitaifa wa Ununuzi kwa njia ya Mtandao
TIN - Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi
TJU - Tangazo la Jumla la Ununuzi
TN - Taasisi Nunuzi
UZM - Ushindani wa Zabuni Kimataifa
UZT - Ushindani wa Zabuni Kitaifa
VAT - Kodi ya Ongezeko la Thamani
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
TANGAZO LA ZABUNI
Namba ya Zabuni: NA.LGA/103/2021/2022/NCS/46 LOT 2
Kwa ajili ya: ZABUNI YA KUFANYA USAFI ,KUKUSANYA TAKA NGUMU KWENYE MAKAZI YA WATU ,MAJENGO YA BIASHARA,MASOKO,STENDI ZA MABASI,MITAA NA OFISI MBALIMBALI KUZOA TAKA NA KUZIPELEKA DAMPO LA SUBIRA NA KUKUSANYA ADA ZA TAKA KATIKA KAYA ZOTE KATA ZA MISUFINI,MATARAWE,BOMBAMBILI KATIKA KAYA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA.
MWALIKO/ TANGAZO LA ZABUNI Tarehe: 18/05/2022
Kwa: WAZABUNI.
Mwaliko huu wa Zabuni (MZ) unafuatia Tangazo la Jumla la Ununuzi (TJU) kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea inapenda kualika zabuni kutoka kwa watu Binafsi, Makampuni, Ushirika, Taasisi au Vikundi vya watu vilivyosajiliwa kisheria wenye nia, uwezo na uzoefu wa ZABUNI YA KUFANYA USAFI ,KUKUSANYA TAKA NGUMU KWENYE MAKAZI YA WATU ,MAJENGO YA BIASHARA,MASOKO,STENDI ZA MABASI,MITAA NA OFISI MBALIMBALI KUZOA TAKA NA KUZIPELEKA DAMPO LA SUBIRA NA KUKUSANYA ADA ZA TAKA KATIKA KAYA ZOTE KATA ZA MISUFINI,MATARAWE NA BOMBAMBILI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA kutuma maombi yao kwa Zabuni hii.
Unaalikwa kuwasilisha Zabuni yako kwa ajili ya kukusanya MAPATO YA KUKUSANYA ADA ZA TAKA kama ilivyoainishwa kwenye Nyaraka za Zabuni.
Zabuni zote zikiwa zimejazwa kikamilifu ziwasilishwe HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA BOX 14 (KITENGO CHA MANUNUZI) kabla ya 13/05/2022 muda kuanzia saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu mchana na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha Zabuni kwa kuzingatia idadi ya siku zilizoruhusiwa kwa Zabuni .Ufunguzi wa Zabuni hizo zitafunguliwa baada ya muda wa mwisho wa kuwasilishwa Zabuni.
Mwombaji aonyesha uzoefu wake kwa mda usiopungua miaka mitatu kazi zinazofanana na kazi tajwa hapo juu.
Mwombaji anatakiwa kuanisha kiasi anachoweza kukuzanya kwa mwei,matumizi pamoja na faida yake na kiasi kitakachobaki halmashauri kwa tarakim na asilimia katika mchanganuo wa mapato na matumizi (kiasi atakachokusanya ,kiasi anachotakiwa apewe kama kamisheni kila mwezi na kiasi kinachobaki halmashauri kila mwezi.
Mwombaji awe na uwezo wa kufanya kazi miezi mitatu bila ya kutegemea halmashauri.
Ada zote zitakusanywa kwa machine za pos zitakazotolewa na kusajiliwa na Manispaa ya Songea.
Mzabuni awe tayari kukusanya ada ya taka kwa viwango vilivyopo katika POS atakazokabidhiwa na Manispaa.
Mzabuni atapaswa kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi,mapato na matumii kila mwisho wa mwezi,kushindwa kufanya hivyo atakuwa amevunja mkataba.
Mzabuni aambatanishe idadi ya watumishi alionao pamoja na vyeti vyao (Mhasibu, Afisa mazingira,Usafirishaji,msimamizi wa Ofisi mmoja).
Mwombaji aambatanishe mwambaji aonyeshe,idadi ya vitendea kazi alivyokuwa nazo mfano:Magari na umiliki wake mitambo na umiliki wake)
Mwombaji awe tayari kununua tayari kununua kitabu kwa tshs.30,000.00 na aambatanishe risiti ya malipo wakati wa kurudisha zabuni.
Zabuni au sehemu za Zabuni ambazo zitawasilishwa nje ya mda au kwa njia isiyoruhusiwa hazitakubaliwa wala kuzingatiwa kwa ajili ya tathmini, bila kujali mazingira yoyote.
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
|
Taasisi Nunuzi (TN) iliyotajwa katika Lohodata ya Zabuni (LDZ) inatangaza zabuni kwa ajili ya kukusanya mapato kama ilivyobainishwa kwenye LDZ na kwenye Jedwali la Mahitaji. Mzabuni Mshindi atatarajiwa kukusanya mapato mahali palipotajwa kwenye LDZ na katika kipindi kilichoainishwa kwenye LDZ kuanzia siku ambayo imetajwa kwenye LDZ.
|
|
Serikali ya Tanzania inakusudia kukusanya mapato na inategemea kwamba sehemu za mapato hayo itatumika kumlipa mtoa huduma wa ukusanyaji wa mapato katika Zabuni iliyotajwa katika LDZ katika mwaka wa fedha uliotajwa katika LDZ.
|
|
Mzabuni anaweza kuwa mtu Binafsi, Kampuni, Ushirika, Taasisi au Kikundi cha watu kilichosajiliwa kisheria au ushirika au ubia baina yao.Kwa suala la ushirika au ubia, washirika au wabia wote watawajibika kipekee au kwa pamoja katika utekelezaji mkataba. Washirika au wabia watachagua kiongozi wao ambaye atakuwa na mamlaka ya kufanya biashara kwa ajili na kwa niaba ya washirika au wabia wengine.
Uteuzi wa kiongozi wa ushirika au ubia utathibitishwa kwa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Mamlaka ya Kisheria iliyothibitishwa na kamishina wa viapo kwa taasisi nunuzi. Makubaliano yoyote yaliyounda ushirika au ubia yaliyothibitishwa na kamishina wa viapo yatawasilishwa kwa TN kama sehemu ya zabuni. Zabuni ya washirika au wabia inapaswa kuainisha majukumu ya kila mbia au mshirika katika mkataba unaopendekezwa. Na kila mzabuni atafanyiwa tathmini au kupekuliwa kulingana na mchango wake tu na wajibu wa kila mbia hautabadilishwa pasipo ridhaa ya kimaandishi ya TN. Mwaliko wa zabuni hii ni kwa wazabuni wanaostahili ambao wametajwa kwenye LDZ. Wazabuni watapaswa kutimiza matakwa ya leseni na usajili ya mamlaka za kisheria za Tanzania. Wazabuni wa nje ya nchi hawaruhusiwi kushiriki zabuni hii. Mzabuni hatakiwi kuwa na mgongano wa kimasilahi. Wazabuni wote watakaobanika kuwa na mgongano wa kimasilahi watakosa sifa ya kushiriki Zabuni hii. Mzabuni hatastahili kuomba au kushinda zabuni hii iwapo: – Mzabuni ametangazwa muflisi; Malipo kwa Mzabuni yamesimamishwa kwa mujibu wa hukumu ya mahakama mbali na hukumu ya kutangaza kufilisika na itokanayo, kwa mujibu wa sheria za nchi, kupoteza kwa ujumla au sehemu haki ya kusimamia na kuondosha mali zake; Michakato ya kisheria imeanzishwa dhidi ya mzabuni inayohusisha agizo la kusimamisha malipo na inayoweza kupelekea, kwa mujibu wa sheria za nchi, kutangazwa kufilisika au katika hali nyingine yeyote itakayopelekea kupoteza kwa ujumla au sehemu haki ya kusimamia na kuondosha mali; Mzabuni amehukumiwa kwa hukumu ya mwisho, ya kosa lolote linalohusisha maadili ya kitaalamu; Mzabuni amefungiwa au amekosa sifa kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 na Kanuni zake za Mwaka 2013, kushiriki katika ununuzi wa umma kwa ajili ya vitendo vya rushwa, kulazimisha maamuzi, kula njama, udanganyifu, kushindwa kuheshimu tamko la dhamana ya zabuni, kukiuka mkataba wa Ununuzi, kuwasilisha sifa za uongo katika mchakato wa Zabuni au vigezo vingine vitakavyoonekana vinafaa na Mamlaka au kampuni imepatikana na kosa la udanganyifu wa taarifa zilizohitajika kwa ajili ya ushiriki katika mwaliko wa zabuni. Mashirika ya Umma au mashirika yanayomilikiwa kati ya Umma na makampuni binafsi yanaweza kushiriki katika zabuni hii, iwapo tu wameruhusiwa kisheria na wanajitegemea kifedha, kama wanafanyakazi chini ya sheria ya biashara, siyo wakala zinazoitegemea Serikali na wamesajiliwa na bodi au mamlaka husika. Wazabuni watawasilisha kwa TN uthibitisho wa sifa zao, uthibitisho wa kukidhi matakwa muhimu ya kisheria, kiufundi na kifedha na uwezo wao na utoshelevu wa rasilimali za kutekeleza mkataba kwa ufanisi. Wazabuni watawasilisha uthibitisho wa sifa zao endelevu kwa kiwango cha kuiridhisha TN, kama TN itakavyowaomba. |
|
Mzabuni ataambatisha nyaraka zifuatazo katika Zabuni:
Nyaraka za usajili wa Mzabuni (mf. kikundi, kampuni n.k.) Fomu ya Zabuni iliyojazwa na kusainiwa ipasavyo; Jedwali la Mahitaji na Bei lililo katika Sehemu ya Nne. lililojazwa na kusainiwa ipasavyo; Leseni halali ya Biashara; Hati Halali ya Usajili wa VAT (kama ipo); Cheti Safi ya Mlipakodi (Tax Clearance Certificate); Orodha ya mikataba iliyotekelezwa ndani ya muda utakaotajwa na TN kwenye LDZ, inayojumuisha majina na anuani za taasisi zilizopokea huduma hizo, kwa ajili ya uthibitisho kama itakavyoainishwa na TN kwenye LDZ; Tamko la Dhamana ya Zabuni; Hati ya Kiapo cha Mamlaka ya Kisheria iliyoidhinishwa (isipokuwa kwa kampuni linalomilikiwa na mtu mmoja (sole proprietor)); Fomu ya Uadilifu iliyo katika Nyaraka za Zabuni iliyojazwa na kusainiwa; Nyaraka nyinginezo zote zitakazohitajika na Taasisi Nunuzi kama zilivyotajwa kwenye Lohodata ya Zabuni (LDZ) |
|
|
|
Marekebisho yoyote, kama yatakuwepo, yanaweza kufanyika kwa kubadilisha zabuni ambayo imekwisha wasilishwa muda wowote kabla ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni kupitia TANePS. Aidha, marekebisho yanaweza pia kufanyika kwa kukata sehemu husika, kuweka saini ya mtu aliyeidhinishwa, tarehe na kuandika kwa usahihi kabla kuwasilisha nyaraka kupitia TANePS, muda wowote kabla ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni; Bei ya zabuni itajumuisha ushuru wote, kodi na ada anazotakiwa kulipa Mzabuni katika Mkataba; Vizio vya kima (unit rates) vilivyotajwa na Mzabuni na kukubalika na pande zote za mkataba, havitabadilika katika kipindi chote cha utekelezaji wa mkataba. Bei zinapaswa kunukuliwa katika Shilingi ya Tanzania (TZS). |
|
Mzabuni atakamilisha kujaza Fomu ya Kuwasilishia Zabuni ambayo imeambatanishwa katika Sehemu ya Nane. Fomu ya Kuwasilisha Zabuni itajazwa kikamilifu bila ya mabadiliko katika muundo wake na hakuna fomu mbadala itakayokubaliwa.
|
|
Malipo yatafanywa katika Shilingi ya Tanzania (TZS).
|
|
Zabuni zitabaki kuwa hai kwa siku [andika siku zisizozidi 120] baada ya siku ya mwisho ya uwasilishaji Zabuni.
|
|
|
|
Endapo itaainishwa kwenye LDZ, Mzabuni anaweza kuwasilisha Zabuni mbadala.
|
|
Isipokuwa kwa kampuni linalomilikiwa na mtu mmoja (sole proprietor), Zabuni itakamilishwa na kusainiwa na mwakilishi aliyeidhinishwa na Mzabuni. Kwa muktadha huu, Hati ya Kiapo cha Mamlaka ya Kisheria itawasilishwa pamoja na Zabuni
Kwa sole proprietor, atatakiwa kuwasilisha nakala ya kitambulisho iliyoidhinishwa na mwakilishi wa Kamishna wa Viapo. |
|
TN itafanyia tathmini na kulinganisha Zabuni kwa namna ifuatayo:
Tathmini ya Awali; ilikutambua ni Zabuni zipi zinakidhi matakwa ya msingi ya nyaraka za Zabuni, kama vile: zilezilizosainiwa kwa usahihi na zilizotimiza vigezo na masharti ya Mwaliko wa Zabuni. Vigezo vifuatavyo vitaangaliwa wakati wa tathmini ya awali: Nyaraka za usajili wa Mzabuni (mf. kikundi, kampuni n.k.) Leseni halali ya Biashara; Cheti Halali Usajili wa VAT (kama ipo) Cheti Safi cha Mlipakodi (Tax Clearance Certificate); Fomu ya kuwasilisha zabuni yenye bei iliyojazwa kikamilifu na kusainiwa ipasavyo sambamba na Jedwali la Mahitaji na Bei; Tamko la Dhamana ya Zabuni; Hati Sanifu ya Kiapo cha Mamlaka ya Kisheria iliyoidhinishwa (isipokuwa kwa kampuni linalomilikiwa na mtu mmoja (sole proprietor); Fomu ya Uadilifu iliyo katika Sehemu ya Nane iliyojazwa na kusainiwa; Uwezo/utayari wa Mzabuni kuwasilisha mapato ndani ya muda uliowekwa kwenye LDZ; nyaraka nyingine zozote zitakazohitajika na TN kama zilivyotajwa kwenye Lohodata ya Zabuni (LDZ) Kama sehemu ya tathmini ya awali, TN itaangalia:
Zabuni zitakazokidhi matakwa ya Nyaraka za Zabuni zitafanyiwa Tathmini ya Kina kwa; Kufanya marekebisho ya makosa ya kihesabu: kama kutakuwa na tofauti ya kimahesabu kati ya kizio cha kima (unit rate) na kiasi (sub-total amount) kilichowasilishwa, basi kizio cha kima kitatumika katika tathimini ya Zabuni na katika Makubaliano ya Mkataba utakaofuata. Kufanya marekebisho stahili, kwa ajili ya mabadiliko yanayokubalika, (variations, deviations) au mabadiliko yanayotokana na kutowekwa kwa baadhi ya vipengele; Kufanya marekebisho stahili kuakisi punguzo la bei ya tuzo au marekebisho mengine ya bei yaliyotolewa; Ulinganishaji wa Zabuni; Katika kulinganisha Zabuni, kamati ya tathmini itaweka kwa kila Mzabuni bei ya Zabuni iliyofanyiwa tathmini ili kubaini Mzabuni mwenye bei kubwa. Mzabuni atakayeoneka na kuwa na bei kubwa baada ya kufanyiwa tathmini, atafanyiwa uhakiki wa uwezo na sifa ili kujiridhisha kwamba ataweza kuingia mkataba na kutekeleza majukumu yake ya mkataba kwa ufanisi. |
|
TN itatoa tuzo ya mkataba kwa Mzabuni ambaye Zabuni yake imeonekana kukidhi vigezo vya Zabuni na ambayo imewasilisha bei ya Zabuni iliyofanyiwa tathmini na kuwa na bei kubwa zaidi.
|
|
Bila ya kuathiri yaliyotajwa hapo juu, TN inayo haki ya kukubali au kukataa Zabuni zote muda wowote kabla ya kutoa tuzo ya Mkataba.
|
|
Kabla ya kutoa tuzo ya Mkataba, TN itatoa Barua ya Kusudio la kutoa Tuzo kwa Wazabuni wote walioshiriki katika zabuni hiyo ikitoa siku saba za kazi kwa Wazabuni hao kuwasilisha malalamiko yoyote (kama yatakuwepo kupitia TANePS. Endapo Mzabuni hatoridhika na maamuzi ya TN, anaweza kukata rufaa kwenye Mamlaka ya Rufaa za Zabuni (PPAA).
|
|
Mzabuni ambaye Zabuni yake imekubaliwa atajulishwa na TN kuwa amekubaliwa kupewa tuzo ya mkataba kabla ya kuisha kwa kipindi cha uhai wa Zabuni.
|
|
Mzabuni mshindi atatakiwa kuwasilisha Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba ndani ya siku kumi na nne (14) za kazi baada ya kukamilika masharti ya kabla ya kusaini mkataba, baada yakupokea barua ya tuzo na kabla ya kusainiwa kwa mkataba. Kiwango na aina ya dhamana hiyo vitatajwa kwenye LDZ na MMM.
Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba itakuwa kwa fedha ya Tanzania katika aina mojawapo kati hizi zifuatazo: Dhamana ya benki au barua ya mkopo iliyotolewa na benki iliyo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayokubalika kwa Mnunuzi, katika muundo uliotolewa katika Mwaliko wa Zabuni au muundo mwingine unaokubalika na Mnunuzi; au Fedha taslimu, hundi halali; au Dhamana ya bima; au Aina nyingine ya dhamana itakayokubalika na Mnunuzi. |
|
Wazabuni wana haki ya kuomba mapitio ya maamuzi ya mchakato wa ununuzi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura namba 410 na Kanuni zake za mwaka 2013 kwenye anuani ya taasisi nunuzi au Mamlaka ya Rufaa za Zabuni (PPAA) ambayo imetolewa kwenye LDZ na nakala ya malalamiko itumwe PPRA kwenye anuani iliyotolewa kwenye LDZ
|
LDZ
|
MKW
|
Maboresho, Mapendekezo, Nyongeza ya Vifungu vya MKW
|
|
1.1
|
Jina la TN: HALMASAHURI YA MANISPAA YA SONGEA
Huduma zitakazonunuliwa ni: Halmashauri ya Manispaa ya Songea inapenda kualika zabuni kutoka kwa watu Binafsi, Makampuni, Ushirika, Taasisi au Vikundi vya watu vilivyosajiliwa kisheria wenye nia, uwezo na uzoefu wa ZABUNI YA KUFANYA USAFI ,KUKUSANYA TAKA NGUMU KWENYE MAKAZI YA WATU ,MAJENGO YA BIASHARA,MASOKO,STENDI ZA MABASI,MITAA NA OFISI MBALIMBALI KUZOA TAKA NA KUZIPELEKA DAMPO LA SUBIRA NA KUKUSANYA ADA ZA TAKA KATIKA KAYA ZOTE KATIKA KATA ZA MISUFINI,MATARAWE NA BOMBAMBILI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA kutuma maombi yao kwa Zabuni hii. Mahali Mapato yatakapokusanywa Ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea : 30% YA MAKUSANYO YOTE YATALIPWA KWENYE AKAUNTI YA HALMASHAURI YA MANISPAA SONGEA. Muda/kipindi cha uwasilishaji wa Huduma: MKATABA UTATEKELEZWA KWA MWAKA MMOJA Tarehe ya kuanza utekelezaji wa mkataba itakuwa 01/07/2022 HADI TAREHE 30/06/2023 |
|
2.1
|
Mwaka wa Fedha: 2021/2022
Jina la Mradi: ZABUNI YA KUFANYA USAFI ,KUKUSANYA TAKA NGUMU KWENYE MAKAZI YA WATU ,MAJENGO YA BIASHARA,MASOKO,STENDI ZA MABASI,MITAA NA OFISI MBALIMBALI KUZOA TAKA NA KUZIPELEKA DAMPO LA SUBIRA NA KUKUSANYA ADA ZA TAKA KATIKA KAYA ZOTE KATIKA KATA ZA MISUFINI,MATARAWE NA BOMBAMBILI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA. Chanzo cha fedha: MAENEO AMBAYO TAKA ZITAKUSANYWA Jina na Namba ya Utambuzi wa Zabuni: LGA/103/2021/2022/NCS/46 LOT 2 |
|
3.5
|
Wazabuni wanaostahili kushiriki ni: KAMPUNI, VIKUNDI AU WATU BINAFSI.
Ukomo wa juu wa Washirika wa pamoja na wabia itakuwa ni: HAKUNA UKOMO. |
|
8.2
|
Barua ya Idhini ya Mtengenezaji: ‘Haitajiki’
|
|
|
Aina ya/za sampuli zitakazowasilishwa pamoja na zabuni: ‘Haitajiki’
Sampuli zitawasilishwa kwa idadi ‘Haitajiki’ Taarifa nyingine kuhusu sampuli ‘Haitajiki’ |
|
1.1(k)
|
Pamoja na nyaraka zilivyotajwa kwenye MKW, nyaraka zifuatazo zitatakiwa kuwasilishwa: HAKUNA
|
|
9.1&9.2
|
Zabuni itakuwa hai kwa muda wa siku 360
|
|
10.1
|
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha zabuni ni: Tarehe: …18/05/2022……………………………..… siku: ………ALHAMISI……………………………… Muda: ……4:00………………………………… |
|
11
|
Zabuni Mbadala “hazikubaliki”
|
|
13.1.(j) na 13.1(d)
|
Nyaraka nyingine ambavyo TN itatumia wakati wa tathmini hamna
Hamna |
|
17.1 |
Kiwango cha Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba: 10%
Aina ya Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba: Tamko la Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba. |
|
|
Hamna
|
|
18
|
HALAMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
Anuani ya PPAA: Katibu Mtendaji, Mamlaka ya Rufaa za Zabuni, S. L. P 9310, DAR ES SALAAM Anuani ya PPRA kwa ajili ya Nakala: Afisa Mtendaji Mkuu, Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma, Ghorofa ya 9, Jengo la Kambarage, Barabara ya PSPF, S. L. P 2865, 41104 DODOMA. |
[Ambatanisha vigezo msawazo (specifications)]
MCHANGANUO WA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWEZI
(Statement of Requirement)
ZABUNI YA KUFANYA USAFI ,KUKUSANYA TAKA NGUMU KWENYE MAKAZI YA WATU ,MAJENGO YA BIASHARA,MASOKO,STENDI ZA MABASI,MITAA NA OFISI MBALIMBALI KUZOA TAKA NA KUZIPELEKA DAMPO LA SUBIRA NA KUKUSANYA ADA ZA TAKA KATIKA KAYA ZOTE KATA ZA MJINI,MFARANYAKI,MAJENGO KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA.
NA.
|
MAELEKEZO YA MAPATO
|
MAPATO
|
JUMLA
|
MAELEZO
|
1a
|
Ada kutoka kwenye makazi ya watu na mitaa
|
|
|
|
1b
|
Ada kutoka kwenye majengo ya biashara ,masoko, stendi za mabasi na ofisi mbalimbali.
|
|
|
|
1c
|
JUMLA
|
|
|
|
|
Maelekezo ya matumizi.
|
Gharama kwa kila moja Tshs.
|
Jumla
|
|
2
|
Mishahara ya wapakiaji taka.
|
|
|
|
3
|
Mishahara ya madereva.
|
|
|
|
4
|
Gharama za mafuta.
|
|
|
|
5
|
Gharama za kulipia dampo.
|
|
|
|
6
|
Gharama za matengenezo ya magari.
|
|
|
|
7
|
Matumizi mengineyo (*)
|
|
|
|
8
|
JUMLA (2+3+4+5+6+7)
|
|
|
|
9
|
1(c)-(8) Fedha inayobaki baada ya kutoa matumizi
|
|
|
|
10
|
Faida (isiyozidi 20% ya fedha zilizobaki baada ya matumizi (namba 9).
|
|
|
|
11
|
Jumla ya gharama za mtoa huduma pamoja na faida yake (8+10).
|
|
|
|
12
|
Fedha anayobaki nayo Mzabuni.
|
|
|
|
13
|
Fedha za halmashauri baada ya kutoa gharama za uendeshaji na faida za mtoa huduma {(IC)-12}.
|
|
|
|
|
MCHANGANUO WA ASILIMIA .
|
|
|
|
14
|
ASILIMIA ITAKAYOBAKI HALMASHAURI 13/1Cx100
|
|
|
|
15
|
ASILIMIA KWA MZABUNI 12/1Cx100
|
|
|
|
|
JUMLA
|
100%
|
|
|
MCHANGANUO WA KAZI ACTIVITY (schedule) NA “TECHNICAL SPECIFICATION”
VIFAA VITAKAVYOTUMIKA KATIKA KATA
SN
|
NAMBA YA MZABUNI
|
AINA YA MAGARI NA MITAMBO
|
01.
|
|
|
02.
|
|
|
NB:
Mzabuni mwenye compactor atapewa nafasi yenye upendeleo kwenye vifaa vinavyohitajikakwenye namba 2 ya sehemu inayoonesha aina ya magari au mitambo.
|
Tafsiri ya maneno
|
|
|
|
“Mkataba” maana yake ni makubaliano yanayofanywa kati ya Mnunuzi na Mtoa Huduma, unaojumuisha maelezo ya mahitaji, mipango, michoro au nyaraka nyingine na masharti yanayoweza kufanyiwa rejea katika Mkataba. Jina la Mkataba limetajwa katika MMM;
“Bei ya Mkataba” maana yake ni bei atakayolipwa Mtoa Huduma ndani ya Mkataba kama gharama ya kutekeleza majukumu yake ya kimkataba kikamilifu na kwa usahihi; “Huduma” maana yake ni ile huduma itakayotolewa kulingana na Mkataba; “Huduma Ambatanishi” maana yake ni zile huduma saidizi zinasaidia uuzaji wa Huduma za Mkataba, kama vile usafirishaji na bima, na huduma nyinginezo ambatanishi, kama vile usimikaji, uanzishaji wa mfumo/mtambo, utoaji wa msaada wa kiufundi, mafunzo, na majukumu mengine ya Mtoa Huduma yanayotajwa kwenye Mkataba; “Mwajiri” maana yake ni Taasisi ya Serikali inayonunua Huduma kama ilivyoainishwa katika MMM. “Mtoa Huduma” maana yake ni kampuni, shirika, taasisi, ubia au mtu binafsi ambao Zabuni yao imekubaliwa na Taasisi Nunuzi na ambaye kwa mujibu wa Mkataba ni upande muhimu au upande wa Mkataba wa ununuzi na TN na ambaye ametajwa katika MMM . |
|
Tafisri ya Mashariti na Nyaraka za Mkataba
|
Katika kutafsiri Masharti haya ya Mkataba, Vichwa vya habari na maelezo ya pembeni yatatumika kwa kadiri inavyofaa na hayatoathiri tafsiri zake isipokuwa pale itakapobainishwa: marejeo ya umoja itamaanisha pia wingi au kinyume chake na jinsi ya kiume inajumuisha pia jinsi ya kike au kinyume chake. Maneno yaliyotumika katika Mkataba huu yatabeba maana zake za kawaida katika lugha za Mkataba isipokuwa pale yanapotafsiriwa vinginevyo.
Nyaraka mbalimbali zinazounda Mkataba; kila waraka utachukuliwa kama unaelezea mwingine. Lakini panapotokea ukinzani, kipaumbele cha nyaraka kitazingatia mpangilio wa nyaraka hizo kama ifuatavyo: Agizo la Ununuzi (ALU); Barua ya Tuzo ya Zabuni; Muhtasari wa Kikao cha Majadiliano (Kama yalikuwepo) Fomu ya Kuwasilisha Zabuni; Masharti Maalum ya Mkataba kwa ajili ya ALU; Masharti ya Jumla ya Mkataba kwa ajili ya ALU; na (Maelezo ya Vigezo Msawazo vya Kiufundi /michoro/ramani kamavipo] Nyaraka zingine zozote zinazounda sehemu ya mkataba kama zilivyoorodheshwa kwenye MMM |
|
Maelekezo
|
Maelekezo yanayotolewa na Mwajiri kwa Mzabuni yatatolewa kwa njia ya maandishi au kwa njia ya kielektroniki na endapo kwa sababu yoyote maelekezo hayo yatatolewa kwa njia ya mdomo, Mtoa Huduma atazingatia maelekezo hayo. Ndani ya kipindi cha siku saba (7), maelekezo hayo ya mdomo yatathibitishwa kwa maandishi au kwa njia ya kielektroniki inayotunza kumbukumbu.
|
|
|
Majukumu ya Msimamizi wa Huduma
|
|
|
Bila kuathiri masharti mengine yoyote, Msimamizi wa Huduma atasimamia utekelezaji wa mkataba kati ya Mwajiri na Mtowa Huduma. Msimamizi wa Huduma hana mamlaka kisheria kurekebisha mkataba.
|
|
|
Mawasiliano
Mawasiliano baina ya pande zinazohusika za Mkataba yatakuwa yamekamilika iwapo tu yatakuwa kwa njia ya maandishi kielektroniki inayotunza kumbukumbu ya yaliyomo ndani ya mawasiliano hayo. Notisi itakuwa imekamilika iwapo tu imewasilishwa kwenye anuani iliyoainishwa kwenye MMM. |
|
Viwango
|
Huduma zinazotolewa chini ya Mkataba zitakidhi viwango vyote na matakwa yaliyoainishwa katika maelezo ya Mahitaji, mipango, michoro, hadidu za rejea au nyaraka nyingine zinazounda Mkataba.
|
|
Matumizi ya Nyaraka na Taarifa za Mkataba
|
Mtoa Huduma hatatoa taarifa yoyote kuhusu Mkataba au kifungu chochote cha mkataba, au maelezo ya Mahitaji, mipango, mchoro, mtindo (pattern) kwa mtu yeyote bila ridhaa ya maandishi ya Mwajiri, isipokuwa kwa mwajiriwa wa Mtoa Huduma ambaye anahusika na utekelezaji wa Mkataba husika. Kutolewa kwa taarifa kwa mwajiriwa huyo kutafanywa kwa kuzingatia usiri na kwa kiwango kinachohitajika katika utekelezaji wa mkataba huo;
Mtoa Huduma hatatumia nyaraka au taarifa zozote zilizoainishwa katika MJM 4.1, bila ya ridhaa ya maandishi ya Mwajiri, isipokuwa kwa malengo ya kutekeleza mkataba; Nyaraka zote zilizotajwa katika MJM 4.1, isipokuwa Mkataba wenyewe, zitabaki kuwa ni mali ya Mwajiri na nakala zote zitarejeshwa, iwapo itahitajika hivyo na Mwajiri baada ya Mtoa Huduma kukamilisha utekelezaji wa Mkataba. |
|
Haki Hataza (Patent Rights)
|
Mtoa Huduma atamlinda Mwajiri dhidi ya madai yote ya upande wa tatu (third party) ya kuingilia hataza, alama ya biashara, au haki ya usanifu inayotokana na utumiaji wa Huduma, matokeo ya huduma, utekelezaji wa kazi au sehemu yoyote ya hayo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
|
Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba
|
Mzabuni mshindi atatakiwa kuwasilisha Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba ndani ya siku kumi na nne (14) za kazi baada ya kupokea barua ya tuzo na kabla ya kusainiwa kwa mkataba.
Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba itatumika kumlipa Mwajiri fidia kwa hasara yoyote inayotokana na Mtoa Huduma kushindwa kukamilisha majukumu yake chini ya Mkataba Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba itakuwa kwa fedha ya Tanzania katika aina mojawapo kati hizi zifuatazo: Dhamana ya benki au barua ya mkopo iliyotolewa na benki iliyondani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayokubalika kwa Mnunuzi, katika muundo uliotolewa katika Mwaliko wa Zabuni au muundo mwingine unaokubalika na Mnunuzi; au Fedha taslimu, hundi halali; au Dhamana ya bima; au Aina nyingine ya dhamana itakayokubalika na Mnunuzi ambayo itatajwa kwenye MMM. Dhamana ya Utekelezaji wa Mkataba itaachiliwa na Mwajiri na kurudishwa kwa Mtoa Huduma si zaidi ya siku thelathini (30) baada ya tarehe ya Mtoa Huduma kukamilisha utekelezaji wa majukumu yake chini ya Mkataba, ikijumuisha majukumu yoyote yanayohusu Kipindi cha Matazamio kilichoanishwa kwenye MMM. Endapo Tamko la Utekelezaji wa Mkataba litatumika badala ya Dhamana, Mtoa Huduma atawasilisha Tamko hilo ndani ya siku kumi na nne (14) za kazi baada ya tarehe ya kutolewa wa tuzo. Endapo Mtoa Huduma atashidwa kutekeleza matakwa ya mkataba, Mwajiri atatoa taarifa kwa Mamlaka akiwasilisha maombi ya Mtoa Huduma Kuchukuliwa Hatua kwa mujibu wa Tamko hilo |
|
Ukaguzi na Majaribio
|
Mwajiri au mwakilishi wake atakuwa na haki ya kukagua na/au kufanya majaribio ya Huduma ili kuthibitisha kama zinaendana na Mkataba pasipokuwa na gharama za ziada kwa Mwajiri. Mkataba utaainisha ukaguzi na majaribio yoyote ambayo Mwajiri atahitaji yafanyike na kuainisha mahali vitakapofanyika. Mwajiri atamtaarifu Mtoa Huduma juu ya utambulisho wa wawakilishi waliochaguliwa kwa ajili ya ukaguzi na majaribio hayo kwa njia ya maandishi au kielektroniki ambayo inatunza kumbukumbu ya mawasiliano;
Ikitokea Huduma yoyote iliyokaguliwa au kufanyiwa majiribio inashindwa kuzingatia Maelezo ya Mahitaji, Mwajirii anaweza kukataa Huduma na Mtoa Huduma atapaswa kutumia njia mbadala au atafanya mabadiliko muhimu ili kufikia matakwa ya Maelezo ya Mahitaji bila gharama yoyote kwa Mwajiri; Hakuna kipengele chochote katika MJM 7 kinachoweza kumruhusu/kumwachilia Mtoa Huduma kutowajibika katika Kipindi cha Matazamio ya Marekebisho au kipindi anatekeleza majukumu mengine chini ya Mkataba huu. |
|
Uwasilishaji Huduma na Nyaraka
|
Uwasilishaji wa Huduma utafanywa na Mtoa Huduma kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika Maelezo ya Mahitaji na Bei. Maelezo ya kina ya bei na/au nyaraka nyingine zitakazo wasilishwa na Mtoa Huduma zimebainishwa katika MMM;
Nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa na Mtoa Huduma zimeainishwa katika MMM na itajumuisha vyeti/hati zinazotolewa na Mwajirii kukubali Huduma zilizotolewa na Mtoa Huduma. |
|
Bima
|
Huduma zinazotolewa, vifaa vinavyotumika, wafanyakazi na vibarua katika Mkataba huu vitakatiwa bima na Mtoa Huduma dhidi ya upotevu, wizi na uharibifu, unaombatana na utoaji huduma kwa namna iliyoainishwa katika MMM.
|
|
Huduma Ambatanishi
|
Mtoa Huduma anaweza kuhitajika kutoa huduma za ziadi kama zilivyoainishwa ndani ya MMM au Mkataba;
Bei ya huduma ambatanishi iliyojazwa kwenye Zabuni au iliyokubaliwa na pande zote mbili (Mwajiri na Mtoa Huduma) itajumuishwa katika Bei ya Mkataba. |
|
|
|
|
Malipo
|
Taratibu na masharti ya malipo yatakayofanywa kwa Mtoa Huduma ni kama yalivyoainishwa kwenye MMM:
Mtoa Huduma ataomba kulipwa na Mwajiri kwa njia ya maandishi au kwa njia ya kielektroniki ambayo inatunza kumbukumbu ya mawasiliano, yakiambatana na Hati ya Madai iikionesha Huduma zilizowasilishwa, Kazi iliyokamilika au huduma zilizofanywa, na nyaraka zitawasilishwa kwa mujibu wa MJM 8, na baada ya kutimiza masharti mengine yaliyoainishwa katika Mkataba; Mwajiri atafanya malipo kwa wakati na kwa ukamilifu kwa idadi ya siku zisizozidi nazilizoainishwa katika MMM baada ya Mtoa Huduma kuwasilisha Hati ya Madai; Malipo yatafanywa kwa Shilingi ya Kitanzania. |
|
Bei ya Huduma
|
Bei zitakazotozwa na Mtoa Huduma kwa Huduma zilizowasilishwa kwenye Mkataba hazitatofautiana na bei zilizowasilishwa na Mtoa Huduma katika Zabuni yake na kukubalika na Mwajiri, isipokuwa pale ambapo marekebisho yoyote ya bei yamefanyika kwa kufuata utaratibu, masharti na vigezo vilivyoidhinishwa kwenye MMM.
|
|
Agizo la Kubadilisha Mawanda
|
Kwa mujibu wa MJM 31 Mwajiri anaweza wakati wowote, kwa agizo la maandishi kwa Mtoa Huduma kufanya mabadiliko ndani ya mawanda ya jumla ya Mkataba katika moja au zaidi ya moja ya mambo yafuatayo:-
|
|
Marekebisho ya Mkataba
|
Kwa kuzingatia MJM 13 hakutakuwa na mabadiliko (variation) au marekebisho (modification) ya masharti ya Mkataba yanayoweza kufanywa isipokuwa kwa marekebisho yaliyosainiwa na pande zote za Mkataba.
|
|
Uhawilishaji (Assignment)
|
Mtoa Huduma hatohamisha jukumu lake la kimkataba iwe lote au sehemu ya majukumu yake kwa Mtoa Huduma mwingine, kabla ya kupata idhini ya maandishi ya Mwajiri.
|
|
Mikataba midogo (Sub-contracts)
|
Mtoa Huduma atamtaarifu Mwajiri kwa maandishi au kwa njia ya kielektroniki inayotunza kumbukumbu ya mawasiliano yaliyofanyika juu ya Mikataba Midogo iliyopewa tuzo chini ya Mkataba huu iwapo haikuelezwa katika Zabuni. Taarifa hiyo katika Zabuni ya awali au baadaye haitamuondolea Mtoa Huduma jukumu au wajibu wake wowote chini ya Mkataba. Mikataba Midogo yote lazima izingatie matakwa ya MJM 2.
Bila kuathiri MJM 16.1, pale ambapo kuna haja ya kuingia mikataba midogo Mtoa Huduma atatoa kipaumbele kwa Makundi Maalum yaliyosajiliwa na yaliyopo kwenye eneo husika, yenye uwezo wa kutoa huduma hiyo. “Makundi Maalum” maana yake ni Makundi yaliyoainishwa kwenye sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410. |
|
Uchel
Matangazo
Habari Mpya
VideoTovuti Mashuhuri
Idadi ya Wasomaji DunianiIdadi ya WasomajiRamani ya MahaliWasiliana nasiSONGEA MUNICIPAL COUNCIL Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA Simu ya Mezani: 025 2602970 Simu ya Kiganjani: Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa |