MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WAKUU WA IDARA WOTE NA WATUMISHI WOTE WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA KUWA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA SONGEA IMERATIBU MAOMBOLEZO YA KIFO CHA RAIS WA AWAMU YA TANO MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI YATAKAYOONGOZWA NA MHESHIMIWA MKUU WA WILAYA SONGEA NA VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI YATAKAYOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 27.03.2021 KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI KATIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA SONGEA.
HIVYO WAKUU WA IDARA, VITENGO NA WATUMISHI WOTE MNATAKIWA KUHUDHURIA MAOMBOLEZO HAYO BILA KUKOSA NA KWA KUZINGATIA MUDA ULIOPANGWA. VAZI LA SIKU HIYO NI NGUO NYEUSI.
IMETOLEWA NA;
MKURUGENZI WA MANISPAA SONGEA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa