TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
UWEKAJI WAZI DAFTARI LA AWALI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA SONGEA MJINI ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA HALMASHAURI YA MANISPAA SONGEA KUWA, ITAWEKA WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA KWA SIKU NNE KUANZIA TAREHE 17 HADI 20 JUNI MWAKA 2020.
UWEKAJI WA DAFTARI UTAFANYIKA KWENYE VITUO VYOTE VILIVYOTUMIKA KWENYE UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA UTAZINGATIA TAHADHARI ZOTE ZA KIAFYA KUHUSU KUZUIA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA COVID- 19 UNAOSABABISHWA NA VIRUSI VYA CORONA.
UWEKAJI WAZI UTAWAHUSISHA WAPIGA KURA WALIOJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MWAKA 2015 NA WALE WALIOJIANDIKISHA WAKATI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA KWANZA MWEZI JANUARI, 2020 NA MWEZI MEI 2020 LAKINI HAWAKUHAKIKI TAARIFA ZAO WAKATI WA UWEKAJI WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA.
MPIGA KURA ANAWEZA KUHAKIKI TAARIFA ZA MPIGA KURA:-
MPIGA KURA ATAFIKA KITUO ALICHOJIANDIKISHA NA KUHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE ORODHA ITAKAYOBANDIKWA KATIKA KITUO HICHO.
KUPITIA SIMU YA KIGANJANI KWA KUPIGA NAMBA *152*00# NA KUFUATA MAELEKEZO.
MPIGA KURA ATAPIGA SIMU NAMBA 0800112100 NA KUFUATA MAELEKEZO YATAYOMUUNGANISHA NA MTOA HUDUMA.AU KUPITIA TOVUTI YA TUME www.nec.go.tz NA KUBOFYA SEHEMU ILIYOANDIKWA UHAKIKI.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UHAKIKI
IWAPO MPIGA KURA AMEHAKIKI TAARIFA NA KUTAKA KUFANYA MAREKEBISHO, ATATAKIWA KWENDA SHULE YA MSINGI MFARANYAKI ILIYOPO KARIBU NA MSIKITI WA WILAYA SONGEA MJINI KUREKEBISHA TAARIFA ZAKE.
MPIGA KURA ANAYETAKA KUMUWEKEA PINGAMIZI MPIGA KURA ASIYE NA SIFA, ATAKWENDA KWENYE KITUO CHA SHULE YA MSINGI MFARANYAKI.
WAPIGA KURA WANATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA NDUGU WALIOFARIKI ILI WAONDOLEWE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.
IWAPO MPIGA KURA ATAHAKIKI TAARIFA ZAKE NA KUBAINI KUWA PICHA YAKE HAIPO, ATATAKIWA KWENDA KWENYE KITUO CHA SHULE YA MSINGI MFARANYAKI ILI APIGWE PICHA NYINGINE.
UWEKAJI WAZI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA HAUTAHUSIKA KUANDIKISHA WAPIGA KURA WAPYA AU KUHAMISHA TAARIFA ZA WAPIGA KURA WALIOHAMA KATA AU JIMBO.
EWE MWANANCHI
KUMBUKA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA KWA KUFUATA MAELEKEZO UTAKAYOPEWA KITUONI ILI KUJIEPUSHA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA ;
AFISA MWANDIKISHAJI
JIMBO LA SONGEA MJINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa