KATIBU Mkuu wa Wizara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Àlisante Ole Gabriel amesema Tanzania ina viwanda zaidi ya 53,000 ambavyo vimechangia kuongeza thamani na kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania.Akizungumza katika kikao kazi cha maafisa Habari na mawasiliano 300 toka nchi nzima kwenye ukumbi wa AICC Jijini Arusha Profesa Gabriel amesema kati ya viwanda hivyo zaidi ya viwanda 3000 vimeanzishwa katika kipindi cha serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli. Kwa mujibu wa Profesa Gabriel kuna aina nne za viwanda ambavyo Anavitaja kuwa ni viwanda vidogo sana ambavyo vinatoa ajira kuanzia mtu mmoja hadi watu wanne ambavyo uwekezaji wake ni kuanzia shilingi milioni tano. Aina ya pili ni viwanda vidogo ambavyo vinatoa ajira kuanzia watu watano hadi 49 ambavyo uwekezaji wake ni kuanzia milioni 200, Viwanda vya kati vinavyoajiri watu kuanzia 50 hadi 99 ambavyo uwekezaji wake ni kuanzia milioni 800 na viwanda vikubwa ambavyo vinatoa ajira kuanzia watu 100 ambavyo uwekezajiwake nI zaidi ya milioni 800.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa