MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo amesema Manispaa ilifuata taratibu zote za kisheria na kanuni kumpata Mkandarasi, Kampuni ya kimataifa ya serikali ya China inayoitwa China Sichuan International Co-operation (SIETCO) ambayo imeanza kazi ya kukarabati barabara za Manispaa ya Songea kwa kiwango cha lami nzito.
Sekambo ametoa ufafanuzi huo kufuatia baadhi ya watu kutoa taarifa potofu kwa baadhi ya wanahabari kuwa Manispaa haikufuata taratibu za kumpata Mkandarasi jambo ambalo ni upotoshaji wa makusudi.
"Hakuna kilichokiukwa katika mchakato mzima wa kumpata Mkandarasi huyu ambaye tayari ameanza kazi kulingana na Mkataba wake'',anasisitiza Sekambo.
Manispaa ya Songea imesaini mkataba na Kampuni ya SIETCO, kukarabati barabara zenye urefu wa kilometa 10.3,Mkataba huo wa miezi 18 unaanza Machi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2019,kwa gharama ya shilingi bilioni 10.96.Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilivunja Mkataba wa ujenzi wa lami nzito yenye urefu wa kilometa 8.6 kati yake na Kampuni ya Lukolo yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam,baada ya Kampuni baada ya Kampuni hiyo kukiuka masharti ya mkataba wa miaka miwili uliomalizika Juni 30 mwaka 2017.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa