Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
30 JUNI 2022
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea vifaa vya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielekroniki (POS) kutoka kwa Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) leo tarehe 30 Juni 2022.
Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Andambike Kyomo (Mchumi) alisema kuwa makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia melekezo ya Serikali kupitia Waziri wa TAMISEMI ambayo yalieleza kuwa “Taratibu za ukusanyaji wa mapato yanayohusiana na ushuru wa maegesho ya magari yaliyokuwa yanakusanywa na TARURA kwa sasa yataanza kukusanya rasmi na mamlaka ya Serikali za mitaa”.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Eng. Wahabu Yahaya Nyamzungu alisema kuwa makabidhiano hayo yamezingatia muongozo wa mgawanyiko wa majukumu ambapo ukusanyaji wa ada ya maegesho ya magari kwa kutumia mfumo wa usimamizi wa mapato ‘TeRMIS’ utasimamiwa na mamlaka za Serikali za mitaa ambapo kuanzia leo Manispaa ya Songea itaanza kutekeleza jukumu hilo.
Aliongeza kuwa TARURA itakuwa na jukumu la kusimamia maeneo ya hifadhi za barabara (Road Reserve) na kupanga maeneo yatakayotumika kwa maegesho ndani ya Mkoa kwa kuzingatia usalama pamoja na kuepusha msongamano wa magari.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa