Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Wakili Bashir Mhoja amewapongeza walimu kutoka shule mbalimbali kwa muitikio mkubwa waliouonesha katika kushiriki kikao cha tathmini ya matokeo ya elimu msingi huku akisisitiza lishe shuleni
Hayo yamejili 08 Desemba 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Songea, kwa lengo la kujadili na kutathmini matokeo ya shule za msingi kwa mwaka 2025.
Akizungumza katika kikao hicho, Wakili Mhoja aliwataka wadau wa elimu na watumishi wa sekta ya elimu kujipanga vizuri ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Aidha, amesisitiza usimamizi madhubuti wa lishe shuleni ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata nafasi ya kufanya vizuri katika masomo. Alieleza pia kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetenga bajeti kwa ajili ya kutoa zawadi kwa walimu wanaofanya vizuri, kama motisha ili kuwahamasisha wengine kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile, amewasihi walimu kuwa makini na wenye weledi katika ufundishaji ili kuhakikisha wanafunzi wanapata ufaulu wa hali ya juu katika masomo yao. Huku akieleza kuwa Wilaya ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kufanya vizuri katika sekta ya elimu ya msingi.
Naye Mwakilishi wa Afisa Elimu msingi Manispaa ya Songea Bi. Monica Barashika aliwasilisha taarifa fupi ya matokeo ya elimu msingi Kwa mwaka 2025 ambapo alibainisha kuwa ufaulu wa mtihani wa elimu msingi Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeshika nafasi ya pili kimkoa huku jumla ya shule msingi 98 zilisajili watahiniwa wa darasa la saba.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea mwaka 2025 imesajili wanafunzi 6639 ambapo 3126 ni Wavulana na 3513 ni Wasichana. Aidha watahiniwa 6429 sawa na (96.8%) walifanya mtihani na watahiniwa 210 sawa na (3.2%) hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali
Alibainisha kuwa jumla ya watahiniwa 5635 sawa na ( 87.64%) wakiwemo Wavulana 2544 sawa na (85.57%) na Wasichana 3091 sawa na (89.4%) wamefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi Kwa mwaka 2025
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepata wastani wa (176.4%) kutoka (166%) ya mwaka 2024. Aidha Halmashauri hiyo imefanya vizuri Kwa ufaulu kiwastani Kwa mwaka 2025 Kwa kupanda Hadi (0.24%) kutoka mwaka 2024
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa