MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefanya ziara ya kukagua mabweni matatu kwa ajili ya ya wanafunzi wasioona katika shule ya msingi Luhira iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mkandarasi wa mradi huo ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo mradi unahusisha ujenzi wa mabweni matatu,vyoo vya ndani ya mabweni vya matundu 18,ukarabati na kuezeka madarasa mawili.Mwakilishi wa TBA amemhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa wanatarajia kukabidhi mabweni hayo yakiwa yamekamilika Machi 22 mwaka huu.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilipokea zaidi ya shilingi milioni 151 toka TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi na ukarabati shule ya Luhira .Mradi huo ulioanza Aprili 2017 ulitarajiwa kukamilika Oktoba 2017.
Taarifa Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa