NIPO Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma naendelea na utafiti wangu,nikiwa katika Kata ya Majimaji nafika hapa nyumbani kwa Diwani wa Kata ya Majimaji Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Simbili Abdalah Makanyaga anazungumzia ongezeko la tembo katika Pori la Akiba la Selous linavyoathiri wananchi wa Kata yake.Kama tunavyofahamu kuwa wilaya ya Tunduru imezungukwa na pori la selous.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Meja Generali Gaudance Milanzi alipotembelea Pori la Selous Kanda ya Likuyuseka wilayani Namtumbo alisema serikali imedhibiti vitendo vya ujangili dhidi ya tembo hali ambayo imesababisha tembo kuongezeka kwa kasi na kuleta changamoto kwa wananchi wanaoishi jirani na hifadhi na mapori ya wanyamapori.
Kutokana na Udhibiti wa vitendo vya ujangili katika Pori la akiba la Selous,matukio ya vifo vya tembo yamepungua kutoka tembo 17 mwaka 2015/2016 hadi tembo nane mwaka wa fedha 2016/2017.Katika kipindi cha Julai 2016 hadi Juni 2017 jumla ya majangili 520 wamekamatwa katika Pori la Selous kutokana na vitendo mbalimbali kinyume cha sheria za Uhifadhi wanyamapori na kanuni zake.
Pori la Akiba la Selous lilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani likiwa pori la kwanza kutengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori barani Afrika na la pili kwa ukubwa duniani baada ya pori la Marekani ambalo linaitwa Yellowstone National Park.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Mwanahabari Mwandamizi kutoka Mkoa wa Ruvuma
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa