IDARA ya Afya katika Manispaa ya songea kwa kushirikiana na wataalam wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanya ukaguzi wa kawaida Aprili 16 katika duka moja la vyakula na vipodozi mjini Songea na kufanikiwa kukamata vyakula na vipodozi ambavyo vimeharibika.
.Afisa Afya na Mratibu wa TFDA Manispaa ya Songea Vitalis Mkomela ametaja thamani ya vyakula na vipodozi vilivyokamatwa kuwa ni Zaidi ya milioni mbili na kwamba Mmiliki amepigwa faini ya shilingi 871,000.Kwa mujibu wa Mkomela matumizi ya vyakula na viodozi vilivyoharibika vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji kwa kuwa kitu chochote ambacho muda wake wa matumizi umepita ni sumu.
Utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wanawake nchini hutumia vipodozi vyenye sumu ambavyo huwasababishia matatizo mbalimbali ikiwemo saratani ya ngozi,figo na kuharibika kwa mimba kwa Mama mjamzito.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa