MAMLAKA ya Udhibiti wa Chakula na Dawa ( TFDA ) katika Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma, imekamata dawa za Binadamu ambazo zilikuwa zinaendelea kuuzwa .
Mratibu wa TFDA katika Manispaa ya Songea, Vitalis Mkomela àmesema dawa za aina mbalimbali zenye thamani ya shilingi 244,000 zilikamatwa katika operesheni maalum ambayo ilifanywa na watalaam wa Idara ya Afya.
Mmiliki wa duka ambalo limekutwa na Dawa hizo amekiri kuuza dawa hizo zilizomalizika muda wake na kwamba tayari amepigwa faini ya shilingi 600,000.TFDA inatoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Songea wanaponunua dawa kusoma kwanza maelekezo yakiwemo yale ambayo yanaonesha dawa zilitengenezwa mwaka gani na tarehe ya mwisho wa matumizi.
Amesema taarifa za raia mmoja ambaye àlikwenda kununua dawa na kubaini aliuziwa dawa ambazo muda wake umemalizika, ndizo zilisaidia TFDA kufuatilia na kufanikiwa kukamata dawa hizo ambazo zinaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu.Amesisitiza kuwa TFDA itaendelea kufanya operesheni za kushitukiza kukagua maduka ya dawa na vipodozi katika Manispaa ya Songea.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa